Ansu Fati Aumia Tena

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Ansu Fati inaelezwa amepata majeraha mengine akiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya huko nchini Marekani.

Ansu Fati ambaye aliitumikia klabu ya Brighton Hove and Albion kwa mkopo msimu uliomalizika msimu huu amerejea ndani ya klabu hiyo kuelekea msimu wa 2024/25, Lakini kwa bahati mbaya amepata majeraha ya mguu ambapo haijafahamika atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.ansu fatiMshambuliaji huyo amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara jambo ambalo limemfanya mpaka kutolewa kwa mkopo ndani ya klabu hiyo, Kwanin alikua ni mchezaji ambaye alitabiriwa makubwa ndani ya Barca mpaka kufikia kupewa jezi ya namba 10 ya Messi lakini majeraha yamekua adui mkubwa wa maendeleo yake ya mpira.

Kocha wa klabu ya Barcelona Hans Flick amethibitisha Ansu Fati kupata majeraha mazoezini na kusema kwasasa timu ya madaktari inampambania aweze kua sawa kwasasa, Lakini kurejea kwake itategemea na muda ambao atautumia katika kujiuguza majeraha yake alisema kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich.

Acha ujumbe