Barcelona Wanaendelea Walipoishia

Klabu ya Barcelona inaendelea ilipoishia kwani leo tena imefanikiwa kushinda mchezo wake wa nne mfululizo kwenye ligi kuu ya Hispania msimu huu baada ya kuichabanga Girona mabao manne kwa moja.

Barcelona wako kwenye ubora msimu huu chini ya kocha wao mpya Hans Flick ambapo mpaka sasa wameshinda michezo yote minne ambayo wamecheza mpaka sasa kwenye ligi kuu nchini Hispania, Hii ikiwa na maana kubwa sana kwa klabu hiyo baada ya kupita kwenye kipindi kigumu misimu kadhaa nyuma.barcelonaBarca walifanikiwa kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa kinda wao hatari Yamine Yamal ambaye amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo, Klabu hiyo ilifanikiwa kwenda kipindi cha mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili kwa bila huku wakicheza mpira wa kuvutia zaidi.

Vijana wa Flick walirejea kipindi cha pili wakiwa na moto uleule wakitafuta mabao mengine zaidi wakipiga hodi kwenye lango la Girona, Ambapo mapema dakika ya 47 ya mchezo Dani Olmo alipiga msumari wa tatu kabla ya kiungo Pedri  kupiga msumari dakika ya 64 huku bao la kufutia machozi la Girona likifungwa na Stuani dakika ya 80.

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Hispania ambapo wamefikisha alama 12, Lakini pia wameondoa uteja wao kwa klabu ya Girona kwani msimu uliomalizika klabu hiyo ilipoteza michezo yote miwili nyumbani na ugenini waliyokutana na Girona.

Acha ujumbe