Klabu ya Barcelona wamekamilisha usajiri wa Jules Kounde na sasa wanaweza kumtumia kwenye michezo ya La liga baada ya chama cha soka nchini humo kuthibitisha kutumika kwake kwenye msimu wa 2022-23.

Kulingana na taarifa iliyotolewa hivi leo, Barcelona wanaweza mjumuisha mchezaji huyo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Real Valladolid.

Barcelona, Barcelona Wakamilisha Usajiri wa Jules Kounde, Meridianbet

Jules Kounde ndio usajiri wa mwisho ukiofanywa na barcelona kwenye majira ya kiangazi na ndio mchezaji wa mwisho kusajiri kwenye kikosi cha Xavi na amepata nafasi hiyo baada ya Umtiti kufanikiwa kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Lecce.

Jules Kounde amesajiriwa kwa kitita chenye thamani £56million, ambapo klabu ya Barcelona walifanikisha dili hilo kwa kuwachenga klabu ya chelsea mabayo ilikuwa tayari kulipa kiasi cha £60million.

Jules Kounde kwenye michezo miwili ya kirafiki wiki hii dhidi ya Pumas na katikati ya wiki dhidi ya manchester City alifanikiwa kupewa jersey ya Umtiti ilihali akiwa bado hajasijiriwa.

Mpaka sasa klabu ya Barcelona imefanikiwa kuwasijiri Raphinha, Robert Lewandowski, Andreas Christensen na Franck Kessie, huku pia wakifanikiwa pia kuwapata mikataba mipya na kuwasijiri kikosini Ousmane Dembele na Sergi Roberto.

Pablo Torre, yeye amesajiriwa kwenye kikosi cha Barcelona B, sio kwenye kikosi cha kwanza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa