WAKATI ligi kuu ikisimama kupisha mechi za timu za taifa, kikosi cha Azam FC kesho kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe ya Zanzibar. 

Azam kwenye michezo miwili ya ligi kuu waliyocheza wamefanikiwa kuvuna pointi nne dhidi ya Kagera Sugar (2-1) na Geita Gold (1-1).

Azam, Azam Kucheza na Taifa Jang’ombe kwa Mkapa, Meridianbet

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa: “Kikosi chetu kinaendelea kufanya maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu unaofuata wa ligi dhidi ya Yanga. 

“Kesho Jumamosi asubuhi timu itaenda Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Jang’ombe.

“Mchezo huo utafanyika siku hiyo hiyo saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar lengo ni Kocha aweze kuwaona wachezaji wake.”

Azam inatarajia kushuka dimbani Septemba 6 mwaka huu kumenyana na Yanga mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Mkapa, Dar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa