UONGOZI wa Pamba FC ya Mwanza umedhamiria kupanda daraja msimu ujao hiyo ni baada ya kusajili nyota wapya kikosini na kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi.

Jana alhamis uongozi ulimtambulisha Kocha wao Mkuu Yusuf Chippo, raia wa Kenya pamoja na benchi zima la ufundi ambalo litaiongoza timu kwa msimu ujao.

Pamba, Pamba Yaitamani Ligi Kuu, Meridianbet

Baada ya utambulisho pia Kocha Chippo amefunguka kuwa mipango ya Pamba ni kupanda ligi kuu hivyo hata yeye malengo yake ni kuipandisha timu hiyo ili aweze kuweka rekodi.

Pamba tayari imeanza kutambulisha wachezaji wao ambapo jana ilimshusha aliyekuwa straika wa Simba, Marcel Kaheza pia leo imemshusha pia Peter Mapunda.

Pamba kwa msimu huu itashiriki michuano ya Championship ambapo takriban kwa miaka 20 timu hiyo haijashiriki ligi kuu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa