KIKOSI cha Singida Big Stars, ambacho kipo Jijini Mwanza kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba FC, Agosti 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Singida Big Stars wameondoka Singida leo kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi ambayo itaendelea baada ya mechi mbili za timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kumalizika.

Singida Big Stars, Singida Big Stars Kujipima na Pamba, Meridianbet

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Singida Big Stars imeeleza kuwa: “kikosi kimeondoka kuelekea Mwanza ambapo kitaweka kambi ya siku 10 mfululizo.

“Awali kambi hiyo ilipangwa kufanyika Mkoani Arusha lakini mabadiliko yamefanyika na kwa sasa kambi hiyo itakuwa mkoani Mwanza.

“Kikosi kikiwa Mkoani Mwanza kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pamba itakayofuatiwa na mechi nyingine ya kirafiki ambayo tutaitangaza baadae.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa