MWENYEKITI wa Simba Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa straika wao mpya raia wa Serbia Dejan Georgijevic ni mchezaji hatari na anatakiwa tumpe muda ili aweze kuonyesha uhatari wake.

Mangungu alisema watu wamekuwa wakimchukulia poa Georgijevic lakini ukweli ni kwamba ni mchezaji mzuri ambaye viongozi na benchi la ufundi hawajafanya makosa kwenye kumsajili kwa kuwa wanajua ubora wake.

Simba, Simba: Yule Zungu Tumpe Muda, Meridianbet

Akizungumzia uwezo wa Georgijevic ambaye amekuwa maarufu kwa jina la ‘mlete mzungu’ alisema kwa sasa anachofanya ni kuendelea kujifunza tamaduni na kuzoea mazingira ya Tanzania na akizoea basi atafanya vizuri zaidi.

“Tuendelee kumpa muda tu, yule mzungu ni mchezaji mzuri viongozi hawawezi kumsajili mchezaji ambaye hajui. Benchi la ufundi nalo haliwezi kuwa linampa nafasi mchezaji ambaye hajui mpira.

“Kwa sasa anajifunza utamaduni mpya na kuzoea mazingira nafikiri baada ya muda atakuwa mtu hatari sana kwa sababu mpira anajua,” alisema.

Dejan tayari ameshaanza kuonyesha kuwa anajua kazi yake ya kufunga kwani tayari ameshaingia kwenye vitabu vya Ligi Kuu Bara na Simba kwa kufunga bao lake la kwanza la ligi, akifanya hivyo baada ya kuwafunga Kagera Sugar kwenye ushindi wa 2-0 wikiendi iliyopita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa