MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally amesema kuwa huenda ni kweli beki Mkenya wa timu hiyo Joash Onyango anaweza akawa amepoteza furaha kwa sasa kwa kuwa amepoteza nafasi ya kucheza.

Ahmed alieleza kuwa Onyango alikuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo na msimu uliopita alikuwa anacheza kwenye kila mchezo na inapotokea kukosa nafasi ya kucheza kwa sasa lazima itakuwa inamuumiza kwa kiasi Fulani.

Akizungumzia ukweli wa kitasa hicho kilichotesa kwa misimu miwili kikiwa panga pangua kwenye timu hiyo akiwa na pacha wake Pascal Wawa aliweka bayana kuwa kila mchezaji anapenda kucheza na ikitokea hachezi lazima asiwe saw ana hilo uenda likawa linamkumba Onyango.


“Inawezekana ikawa kweli Onyango amepoteza furaha kwa sababu hana nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kama ambavyo tumeona kwenye mechi hizi za mwanzo. Nafikiri kweli ikawa hana furaha ndani yake.

“Kila mchezaji anapenda kucheza na kwa Onyango yeye alikuwa ni panga pangua kwenye kikosi, sasa hivi hachezi tena naamini hawezi kuwa sawa,” alisema.

Onyango amekuwa akipata ugumu wa kucheza mbele ya wachezaji wanaoanza sasa Mohamed Outtara na Henock Inonga Backa ambao kwa sasa wamekuwa ndiyo nguzo ya safu ya ulinzi ya Simba.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa