Kiungo wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa imepanga kumtoa kwa  mkopo kiungo wake Leandro Parades kwenda klabu ya Juventus ya nchini Italia, Kiungo huyo raia wa Argentina ameonesha nia kwa klabu yake anaihitaji Juventus kama chaguo la kwanza.

Inaelezwa kiungo huyo alishakua na makubaliano ya maslahi binafsi na wababe hao wa Italia wiki kadhaa nyuma.

parades, Leandro Parades Kutolewa kwa Mkopo Juventus., MeridianbetKlabu zote mbili zimeoneshana kukubaliana na dili hili huku kila pande wakijaribu kusukuma dili hili likamilike kwa wakati. klabu ya Juventus inataka kumchukua kiungo huyo kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na kipengele cha kumnunua jumla.

Kiungo wa uzuiaji huyo aliewatumikia mabingwa  hao kwa takribani misimu minne na anaondoka klabuni hapo kwaajili ya kupata nafasi zaidi ya kucheza kuelekea michuano ya kombe la dunia mwishoni mwa mwaka huu kule nchini Qatar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa