Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Newcastle United kwajili ya kumsajili golikipa wake namba mbili kwa mkopo Martin Dubravka.

Man United inafikiria kutafuta kipa mwingine ili kuja kutoa changamoto kwa makipa wa klabu hiyo David de Gea pamoja na Tom Heaton haswa golikipa namba moja David ambae inaelezwa kiwango chake kimekua sio cha kuridhisha hivi karibuni.

united, United Yamnyemelea Kipa wa Newcastle., MeridianbetPamoja na hivyo inaelezwa kuwa mwalimu  anatafuta pia golikipa ambae ataweza kuendana na mfumo wake kitu ambacho kimeonekana kua sugu kwa golikipa namba moja wa United David de Gea.

Kazi inaweza kua nyepesi pia kwa upande wa United kwasababu kipa huyo amekosa nafasi klabuni Newcastle baada ya ujio wa golikipa mpya Nick Pope alietokea Burnley iliyoshuka daraja na kua chaguo la kwanza la mwalimu Eddie Howe. Hali hii imemfanya golikipa Martin kufikiria kutafuta changamoto sehemu nyingine.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa