Klabu ya ya wanawake ya Simba inayojukijana kama Simba Queens imefankiwa kutinga fainali katika michuano ya afrika mashariki na kati maarufu kama Cecafa.

klabu ya wanawake ya Simba iliweza kuifunga timu ya As Kigali jumla ya mabao matano kwa moja kwenye nusu fainali hiyo mchezo ukipigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Simba Queens wanafanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kucheza mechi tatu kwenye hatua ya makundi na kutoa kipigo kwenye mechi zote tatu.

simba queens, Simba Queens Yatinga Fainali Cecafa., MeridianbetMabingwa hao mara tatu mfululizo wa ligi kuu ya wanawake Tanzania wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyto na wataenda kumenyana na klabu ya Uganda inayojulikana kama She Corporate ambayo ilishinda mchezo wake wa nusu fainali pia siku ya jana dhidi ya klabu ya CBE FC ya nchini Ethiopia.

Mhezo huo wa fainali kati ya Simba Queens dhidi ya She Corporate unatizamiwa kua mchezo mzuri na wa kuvutia kwani klabu hizo zilishakutana kwenye hatua ya makundi na Simba Queens kushinda bao mbili kwa bila.

Licha ya Simba Queens kushinda mchezo lakini klabu hiyo toka Uganda ilionesha ushindani mkubwa hivo fainali hiyo inatizamiwa kua yenye mvuto wa aina yake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa