KIKOSI cha Simba kimewasili nchini Sudan kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na AL Hilal.

Michezo hiyo ya kirafiki itapigwa nchini Sudan ambapo mechi ya kwanza dhidi ya Asante Kotoko itachezwa Agosti 28, mwaka huu na ile ya Al Hilal itakuwa Agosti 31, mwaka huu.

Simba, Simba Yatua Sudan Kibabe, Meridianbet

Akizungumza baada ya timu kuwasili nchini Sudan, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa: “Tunashukuru timu imewasili salama na leo tutafanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa.

“Kesho pia timu itafanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Asante Kotoko, mechi hizi zitakuwa kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi pamoja na ile ya kimataifa.

“Tumeondoka na jumla ya wachezaji 19 tu ambao tulikuwa nao kambini lakini amekosekana Sadio Kanuti ambaye anashughulikia masuala ya Passport yake pia na wale wachezaji waliopo timu ya taifa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa