Nyota wa zamani wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero amemtania mlinzi Nicolas Otamendi kwa kumkanya kutokumchezea vibaya nyota wa timu ya taifa ya Argentina Leo Messi kwa sababu anahitajika kwenye michezo ya kombe la dunia mwaka huu nchini Qatar.

Messi kwa sasa anaichezea timu ya PSG huku Otamendi yeye akiichezea Benfica amba po kwenye mashindano ya Ulaya wamepangwa kundi moja ambapo wanatarajia kukutana kwenye michezo miwili ya kundi H, huku kikiwa na timu za PSG, Benfica, Juventus na Maccabi Haifa.

Sergio Aguero, Sergio Aguero Amuonya Nicolas Otamendi, Meridianbet

Sergio Aguero akizungumza kwenye Channel yake ya Twitch, alimuomba Otamendi asimfanyie madhambi nyota huyo watakapo kutana kwenye michezo ya klabu bingwa barani ulaya kwani wanamtegemea kwenye michezo ya kombe la dunia.

“PSG, Juventus, Benfica, Otamendi atakwenda kuwapiga watu viatu. Otamendi yupo Benfica , kwaiyo ataanza kufanya vurugu zake na atakutana na messi. Usimumize messi , kwa sababu nitakuua. Kombe la dunia linakuja, Ota.’

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa