Bernardo Silva kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno anaezungumzwa kuondoka klabuni hapo.

Imekua ikielezwa mara kadhaa kiungo huyo wa kireno ataihama klabu hiyo na klabu inayoytajwa zaidi ni miamba kutoka nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona ambayo imekua ikimuwinda kiungo huyo kwa muda mrefu lakini leo hii kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amefunguka kua mchezaji huyo hataondoka klabuni hapo licha ya kutambua kua kuna klabu kadhaa zinamuhitaji mchezaji huyo ikiwemo klabu ya Barcelona.

bernardo silva, Bernardo Silva Kusalia City., Meridianbet

Pep ameeleza Bernardo atasalia City na hawana mazungumzo na klabu yeyote kumuhusu mchezaji huyo.

Siku kadhaa nyuma pia mtendaji wa klabu hiyo Ferran Soriano alieleza hawana mpango wa kumuachia mchezaji huyo kwenda klabu yeyote kwani ni mchezaji muhimu kwenye timu hiyo na bado yupo kwenye mipango ya mwalimu.

Hii si mara ya kwanza kwa Bernardo kuhusishwa kuondoka klabuni hapo ila dirisha likifungwa anasalia kua mchezaji wa City.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa