Deco: Hatujamsajili Nico Williams kwakua Tuna Wachezaji Bora

Mkurugenzi wa klabu ya Barcelona na nyota wa zamani wa klabu hiyo Deco amesema hawajamsajili winga wa klabu ya Atletico Bilabo kwakua wana wachezaji wengi wenye ubora katika klabu hiyo.

Deco amesema hawakumsajili Nico Williams kwasababu wana wachezaji bora kama Raphinha, Ferran Torres, Ansu Fati, Lamine Yamal, Fermin Lopez, pamoja na Dani Olmo hivo kutokana na ubora wa wachezaji hao ambao wanao kikosini ndio sababu ya wao kutokumsajili mchezaji huyo kutoka Athletic Bilbao.decoDeco  ameongeza kwa kusema Dani Olmo ambaye wamemsajili kutoka klabu ya Rb Leipzig anaweza kuwapa machaguzi mengi zaidi kikosini kwakua ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja kiwanjani, Hivo ni usajili bora kwao kuliko kusajili winga mmoja tu.

Ikumbukwe kwenye dirisha kubwa lililopita klabu ya Fc Barcelona ilikua ikimfuatilia kwa karibu winga Nico Williams kutoka klabu ya Athletic Bilbao, Lakini dili hilo lilifeli na sababu kubwa iliyoelezwa ni klabu ya Barca kutokua na kiwango ambacho Bilbao walikihitaji na maslahi kwa upande wa mchezaji.

Acha ujumbe