Kocha mkuu wa Aston Villa Unai Emery anawafukuzia wachezaji wawili wa Real Madrid Eden Hazard na Nacho Fernandez ili aweze kuwanunua katika dirisha dogo la mwezi Januari.
Kocha huyo ameanza vyema tangu kuchukua nafasi ya Steven Gerrard hapo Villa Park baada ya kupata ushindi mara mbili mfululizo kwenye Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United na Brighton.
Emery ana nia ya kuongeza ubora kwenye kikosi chake huku ripoti kutoka nchini Uhispania zikipendekeza Hazard na Nacho wote wataruhusiwa kuondoka Los Blancos katika dirisha la majira ya baridi.
Hazard ambaye ana miaka 31 na ambaye alifanya vizuri akiwa na Chelsea, hajawahi kuonekana kufurahia katika mji mkuu wa Uhispania na kiwango chake cha kudhoofisha kimemfanya akose namba kwenye kikosi cha Ancelotti.
Mbelgiji huyo alisajiliwa kwa ada ya awali ya pauni milioni 89 pamoja na nyongeza anaweza kupatikana kwa pauni milioni 22. Villa walifanikiwa kumaliza dili kama hilo kwa mchezaji wa Barcelona Philippe Coutinho lakini watalazimika kuzuia nia ya vilabu kama Newcastle kumnunua Hazard.
Nacho mwenye miaka 32, mkataba wake unamalizika msimu wa joto na pia anaripotiwa kupatikana kwa ada iliyopunguzwa huku kocha wa Real Carlo Ancelotti akiwa tayari kulipwa.
Beki huyo mahiri ametumia miaka 21 Santiago Bernabeu tangu ajiunge na akademi ya klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 11 na angeweza kuleta uzoefu na uwezo wa kiufundi kwa Emery.
Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA