Kocha mpya wa klabu ya Aston Villa Unai Emery ameanza vizuri ndani ya klabu hiyo baada ya kuifunga klabu ya Manchester United mabao matatu kwa moja katika dimba la Villa park.

Aston Villa chini ya Unai Emery wameweza kuifunga Manchester United ambayo ilicheza michezo tisa bila kufungwa katika michuano yote, Lakini katika mchezo wa leo dhidi ya Aston Villa wameweza kuruhusu kufungwa.unai emeryKlabu ya Aston Villa iliweza kupata magoli mawili ya haraka ndani ya Dakika tano kupitia kwa Leon Bailey aliefunga dakika ya 5 kabla ya Lucas Digne kufungwa kwa mkwaju wa faulo dakika ya 11 ya mchezo na kuwaweka wenyeji mbele kwa mabao mawili.

Klabu ya Manchester United wao walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa beki wa kushoto Luke Shaw dakika ya 45 ya mchezo, huku mchezo ukienda mapumziko kwa mabao mawili kwa moja Villa wakiwa mbele.

Kipindi cha pili kilianza United wakionekana kutaka kusawazisha kabla ya Jacob Ramsey kufunga bao la tatu na la mwisho katika mchezo huo dakika ya 49 ya mchezo, Na mchezo huo kumalizika kwa Aston Villa kushinda mabao matatu kwa moja.unai emeryKocha Unai Emery anatarajiwa kufanya vizuri na timu hiyo kutokana na uzoefu wake kwenye ligi hiyo, Pia uwezo wake wa kufundisha soka pamoja na mwanzo mzuri alioanza nao.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa