Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Anchelotti ameweka bayana kua klabu hiyo haina mpango wa kufanya usajili wowote kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Kocha huyo ameeleza hayo kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Rayo Vallecano ugenini, Anchelotti amekua akisistiza jambo hilo mara kadhaa na hii inatokana na klabu hiyo kuhusishwa na wachezaji kadhaa.anchelottiKocha huyo amekua akiamini kikosi cha klabu hiyo kimeimarika na kina wachezaji wa kujitosheleza kabisa na wenye ubora wa hali ya juu, Huku dirisha lililopita klabu hiyo kuongeza mchezaji mmoja tu ili kuboresha kikosi hicho.

Klabu ya Real Madrid imekua ikifanya kazi ya kuongeza mikataba kwa wachezaji wake nyota klabuni hapo kama Karim Benzema, Luca Modric na wengine wakiwa kwenye mazungumzo.anchelottiKocha Anchelotti ambae amefanikiwa kuipatia klabu hiyo taji la 14 la ulaya huku yeye akifikisha mataji manne na kuweka rekodi kua kocha wa kwanza kufanya hivyo, Anaamini klabu yake ipo kwenye wakati mzuri na ina wachezaji wazuri hivo haina haja ya kuingia sokoni mwezi Januari kwajili ya kukiinarisha kikosi chao.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa