Arsenal Mwendo Mdundo Yaibamiza Chelsea Darajani

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuvunja daraja baada ya kuivurumisha klabu ya Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani kwa bao moja kwa bila, ambapo washika mitutu hao wa London wakirejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Klabu ya Arsenal wamefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo mgumu ambao ulikua unachezwa kwa tahadhari kubwa kwa pande zote mbili, Lakini vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza walioweza kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.arsenalKatika mchezo huo uliokua mgumu ni beki Gabriel aliowapatia washika mitutu hao wa London bao la ushindi baada ya mpira wa kona uliopigwa na Bukayo Saka, na kuwafanya kufikisha alama 34 baada ya kucheza michezo 13 na kuwashusha klabu ya Manchester City walioongoza kwa muda.

Klabu ya Chelsea wao wanaendelea kuteremka baada ya kufungwa mchezo huo kwani wameshuka kutoka mafasi ya 6 mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.arsenalKlabu ya Arsenal wao tayari wameshacheza na vigogo karibia wote kasoro klabu ya Manchester City,huku wakipoteza dhidi ya Manchester United huku wakiwa wameshinda michezo yote na kujihakikishia mazingira mazuri ya kubaki kileleni mpaka kuelekea mapumziko ya kombe la dunia.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

Acha ujumbe