Sio mara ya kwanza msimu huu, mchezaji wa Ral Madrid Vinicius Jr amekuwa akilengwa na unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi alipokuwa akitimiza majukumu yake.

Mnamo Septemba, alibaguliwa vibaya wakati wa ushindi wa 2-1 wa Los Blancos dhidi ya Atletico Madrid kwenye dabi ya Madrid.
Siku ya Ijumaa, mashabiki wa Real Valladolid walirekodiwa wakielekeza kelele kwa Mbrazil huyo (Vicius Jr) alipokuwa akitembea kuzunguka uwanja mbele ya sehemu ya nyumbani. Kufuatia mechi hiyo.
Vicius Jr mwenye umri wa miaka 22 aliilenga La Liga kufuatia tukio hilo, akitaja kutochukua hatua kutoka kwa bodi inayosimamia ligi hiyo juu ya matukio ya ubaguzi wa rangi.
Real Valladolid sasa wametoa taarifa kufuatia tukio hilo la Ijumaa, ambapo walielezea kusikitishwa kwao na kitendo cha mashabiki wao, na kuthibitisha kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika.
“Real Valladolid inalaani kabisa aina yoyote ya ubaguzi wa rangi na inajutia sana kilichotokea (kwenye mechi ya Real Madrid). Klabu, bila shaka, iko tayari kushirikiana na LaLiga kufanya uchunguzi husika, na inahifadhi haki ya kuchukua hatua za kinidhamu endapo kutakuwa na wasajili wanaohusika katika matukio hayo.
Klabu hiyo pia kwamba hatua zinachukuliwa ili kuepusha matukio ya aina hiyo kutokea kwenye klabu tena siku zijazo.
“Hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi katika mpira wa miguu na jamii, kwa hivyo Real Valladolid imedhamiria kutekeleza hatua zaidi na zaidi za kuongeza ufahamu, kuepuka na kupambana na matukio yoyote sawa.
“Matukio haya ya pekee hayawakilishi idadi kubwa ya mashabiki wa rangi nyeupe na zambarau, wenye heshima kila wakati, na washiriki wa jana katika onyesho zuri katika viwanja vya Zorrilla.” Taarifa ya Klabu ilisomeka hivyo.

