Pedri Apata Majeraha Tena

Kiungo wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Pedri Gonzalez inataarifiwa atakua nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kupata majeraha ya nyama za paja.

Kiungo Pedri amegundulika kua ana majeraha ya nyama za paja hivo anaweza kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne mpaka sita jambo ambalo linaenda kua pigo kwa klabu ya Barcelona tena kwenye safu ya kiungo.PedriKiungo huyo sasa inakua kama mwendelezo kwa yeye kupata majeraha kwani msimu uliomalizika alikaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu, Hivo hii imekua muendelezo wa majeraha kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania.

Kiungo huyo amekua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Barca kutokana na ubora ambao amekua akionesha tangu amepata nafasi kwenye timu ya kwanza akitokea kwenye akademi ya klabu hiyo inayofahamika kama La masia.PedriKiungo fundi Pedri ameibua hofu kutokana na hali inayomkabili kwasasa ya kupata majeraha yanayojirudia, Kwani umri wake bado mdogo na wachezaji wadogo ambao walifanya vizuri halafu wakaanza kundamwa na majeraha wengi walipotea kwenye ramani ya soka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.