Klabu ya Real Madrid imepata matokeo ya ushindi mapema leo katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania wa mabao matatu kwa moja baada ya kutoka kusuluhu dhidi ya Real Betis mchezo uliomalizika.
Klabu ya Real Madrid leo imeweza kupata ushindi mzuri wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Santiago Bernabeu huku wakitanguliwa kwa goli la mapema kupitia kwa Joselu alieifungia Espanyol, Lakini vijana wa Ancelotti walitulia na kusawazisha kupitia kwa Vinicius Jr.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Hispania walifanikiwa kuutawala mchezo baada ya kusawazisha bao kupitia Vincius kabla ya beki wa kimataifa wa Brazil Eder Militao kuwapatia bao la uongozi mnamo dakika ya 39 ya mchezo na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa moja.
Klabu ya Real Madrid ilirejea kipindi cha pili ikiwa inaonesha ina kiu kubwa ya kutaka kuongeza mabao kwani walifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, Lakini hawakufanikiwa mpaka pale dakika ya 93 zikiwa za nyongeza Marco Asensio akiwapatia bao la tatu klabu hiyo na mchezo kumalizika kwa mabao matatu kwa moja.Real Madrid baada ya kushinda mchezo huu wamefanikiwa kufikisha jumla ya alama 56 baada ya kucheza michezo 25, Huku wakiwa nyuma kwa alama 6 kwa vianara wa ligi hiyo klabu ya Fc Barcelona ambao wamekua na wakati mzuri sana ndani ya msimu huu.