Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka nchini Afrika ya Kusini wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kishindo kikubwa baada ya kuifunga klabu ya Al-Ahly mabao matano kwa mawili.
Mamelodi Sundowns ambao wamecheza mchezo wao wa nne wa kundi leo wakiwa wamebakiza michezo miwili tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Hii imekuja baada ya klabu hiyo kufikisha alama 10 kwenye kundi lake wakiwa tayari wameshashinda michezo mitatu.Mabao ya Mamelodi Sundowns yalifungwa na Allende alieipatia klabu hiyo bao la kuongoza mapema dakika ya nne ya mchezo kabla ya Mohamed Sherif kusawazisha dakika ya 13, Mvua ya mbao ilianza kumininika bao lapili likifungwa na Zwane, Mokoena akiweka la tatu kabla ya Shalulile kuweka mawili na kukamilisha idadi huku bao la pili la Ahly likifungwa na Percy Tau.
Klabu hiyo kutoka kusini mwa Afrika imekua mwiba mkali kwa klabu ya Al-Ahly miaka ya hivi karibuni kwani wamekua wakitoa kipigo kikubwa kwa mabingw ahao wa muda wote barani Afrika, Mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Cairo ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili lakini leo Ahly wamepokea kipigo kizito.Mamelodi Sundowns wamekua kwenye kiwango bora mpaka sasa kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika kwani mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo mitatu kati ya minne waliyocheza huku wakisuluhu mchezo mmoja, Hii inaonesha moja kwa moja klabu hiyo ina dhamira kubwa na michuano hiyo msimu huu.