Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amempakulia minyama kiungo wake raia wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie De Jong kua ni moja ya wachezaji bora duniani kwasasa.
Kocha Xavi amemsifia Frenkie De Jong ikiwa ni baada ya kutokuanza vizuri baina yake na kiungo huyo ndani ya viunga vya Camp Nou, Kwani kocha huyo hakua akimtumia De Jong mara kwa mara.
Taarifa zinaeleza kua kocha huyo ambaye amewahi kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji alikua havutiwi na Frenkie De Jong, Huku ikifika hatua ya kuruhusu kiungo huyo auzwe japo kiungo huyo aligoma kuondoka klabuni hapo.
Kocha Xavi Hernandez amegeuka kua shabiki mkubwa wa kiungo huyo na kusema ni moja ya wachezaji wenye uwezo wa kitofauti kuanzia kwenye kiwango cha mazoezi, Wakati mwingine wanaomuona kwenye kiwanja cha mazoezi wanajiuliza kwanini Frenkie anakosolewa sana.
Kiungo Frenkie De Jong amekua akionesha uwezo mkubwa ndani ya klabu ya Barcelona tangu aaminiwe na kocha huyo, Huku akigeuka kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Barcelona.

