Katika siku ambazo wapenzi wengi wa soka hupenda kuziona ni pale miamba wa soka na wenye tambo nyingi juu ya mapato yao na uzuri wa vikosi vyao wanapokutana kwenye mchezo. Imekuwa kawaida sana kwa wawili hao kukutana na kihistoria hawa ni mahasimu wakubwa ambao kuna wakati hata upinzani wao huweza kuhusishwa kidogo na mambo ya kisiasa kitu ambacho kimekuwa kikileta radha nzuri kwenye soka lao.
Ni juzi tu wawili hao walipokutana katika mchezo wao wa Copa del Rey na kushuhudiwa meli ikizama katika bandari ya nyumbani mwa Barcelona kuondoka na ushindi mnono uliomfanya kukaa kileleni kihistoria pindi wawili hao wanapokutana na matokeo yao yanavyokuwa. Madrid hajawa na ubora wa kuridhisha hivi karibuni kitu ambacho bado kinaonekana kabisa kwamba msimu huu ni wa Barcelona.
Imekuwa ni timu ambayo haipo kiushindani sana pamoja na kuwa na kikosi chenye wachezaji waliotumikia kikosi hicho kwa kipindi kirefu sana lakini suala hilo linaonekana kitaalamu kwamba wachezaji waliopo wamekaa kwa kipindi kirefu mno na kushinda kila aina ya kikombe wanachostahili hivyo ili kuleta ushindani inapaswa kuwepo kwa kikosi kipya chenye njaa ya mataji ili kutafuta heshima iliyowekwa na wenzao.
Kwa nidhamu ya soka ilivyo Madrid leo anamkaribisha Barcelona katika ardhi yake kwa mara ya pili ndani ya wiki suala ambalo linamlazimisha kufuta uteja wake wa kupoteza kwa mara ya tatu tena; kitu ambacho sioni kama mashabiki wataendelea kuwa na uvumilivu nacho isitoshe mechi hiyo ni sehemu ya ligi yao.
Inafahamika heshima ambayo mechi za wawili hao zinavyokuwa kutokana na kutawaliwa kwa ufundi mkubwa, tahadhari na tambo nyingi ambazo huwa na nia ya kuchochea soka safi. Kutokana na uwezo wa vikosi hivyo katika kutafuta matokeo yaliyo bora kabisa na yenye tija mbele ya mashabiki zao.
Barcelona wanajivunia kuwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu kama Messi, Suarez, Raktic, Dembele na wengineo ambao bila shaka wamekuwa wakikipa ushindi mara nyingi kikosi chao pia hata wachezaji wanaokaa benchi ni wale wenye wasifu mkubwa sana hata wanapopewa nafasi ya kuingia uwanjani.
Kwa upande wa Madrid kuna wachezaji kama Modric, Vazquez, Isco, Casemiro lakini wamekuwa wakikosa mtu anayeweza kulazimisha matokeo pindi kikosi hicho kinapokuwa kinaelemewa. Japo wao hawataki kabisa kuhusisha hali yao na sasa na kukosekana kwa Ronaldo ndani ya kikosi chao hicho.
Katika mechi hiyo kuna vitu bado havizuiliki tutaendelea kumwona Messi na Barcelona yake wakiendeleza ubabe mbele ya Madrid ambao bado wanasuasua kupata matokeo mazuri yenye kushawishi ushindani wao.

