Yanga Yaanza Mabadiliko Kwa 100%

Baada ya safari ndefu ya timu ya Yanga, huku wakipitia safari ndefu yenye milima, mabonde, jua kali, mvua nyingi ila bila kukata tamaa, hatimaye Yanga imefanikiwa kufikia mabadiliko katika klabu yao.

Safari ya mabadiliko ya Yanga ilianza kwa kuwa katika ILANI ya UCHAGUZI ya M/Kiti Dr. Mshindo Msolla na hatimaye kuunda kamati ya mabadiliko chini ya mwanasheria msomi ALEX MGONGOLWA.

Kazi kubwa ilifanyika na kwa USHAURI mkubwa wa LALIGA katika kupitia mfumo imara (STABLE ), wa muda mrefu ( LONG TERM ), wenye malengo mazuri (RESULT ORIENTED) na wenye uhalisia wa kitanzania (CUSTOMIZED).

Katika chapisho la Instagram la muwakilishi wa wadhamini wa Yanga SC, engineer Hersi, yaliainishwa Maeneo yaliofanyiwa kazi katika mabadiliko, ambayo yanajumuisha ;

1. Umiliki wa klabu – CLUB OWNERSHIP
2. Muundo wa klabu – STRUCTURE OF ADMINISTRATION.
3. Ushirikishwaji wa wanachama na mashabiki – FAN ENGAGEMENT

Aidha, kuelekea kwenye mabadiliko ya klabu, yako maeneo mengine yatahitaji kupitiwa kupitia dirisha la mabadiliko.

1. Football development
2. Legal and complience
3. Financial controls
4. Marketing
5. Communication
6. Sales

Mfumo huu uliopitishwa leo katika klabu hii kongwe nchini, unaenda kuwa mfumo bora barani AFRICA na wa kuigwa na vilabu vingine.

Elimu kwa wanachama kupitia matawi na vikundi maalum vilipata nafasi ya kujifunza mfumo na kutoa mapendekezo yao ambayo leo hii yanakwenda kuijenga YANGA MPYA.

Aidha mwenyekiti huyo wa udhamini amepeleka shukran zake kwa Dr. Mshindo Msola na kamati nzima ya Sekretariet kwa kuamini kuwa Yanga inaweza kupitia mabadiliko, Alex Mgongolwa na Raymond Wawa ambao walikuwa ni wenyeviti wa kamati ya mabadiliko na katiba.

Vile vile, Hersi alitaka kutoa shukran zake kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hii KONGWE kwa kutoa BARAKA zao kuelekea mabadiliko ya mfumo.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

United, United Wakutana na Mawakala wa Camavinga, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.