Klabu ya wananchi maarufu kama Yanga imefanikiwa kusaini kandarasi ya miaka 10 ya haki za matangazo kupitia channel ya Yanga TV na Azam Media ambao una thamani ya bilioni 41.
Afisa mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando na Mwenyekiti wa Young Africans SC, Dkt. Mshindo Msolla, wamesaini mkataba wa mashirikiano ya maudhui wenye thamani ya Shilingi bilioni 41 pamoja na VAT kwa kipindi cha miaka 10.

Katika mkataba huo, klabu ya wananchi itakuwa ikipokea kiasi cha shiliingi milioni 200 kila mwezi kama pesa ya mkataba na pia endapo Yanga watashika nafasi mbili za juu kwenye VPL, basi Azam Media watatoa bonasi ya shilingi bilioni 3.
Hii inakuwa ni historia nyingine inaandika na Azam Media baada ya hivi karibuni kusaini mkataba na TFF uliokuwa na thamani zaidi ya bilioni 225.6.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

