Kocha wa timu ya Taifa ya wanawake ya Uholanzi – Sarina Wiegman amechaguliwa kuwa mrithi wa Phil Neville kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake – Uingereza.
Kibarua cha Neville kinakwisha mwezi Julai, 2021 na Sarina anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kunako michuano ya Women’s Euro 2021 ambayo imesogezwa mbele mpaka Julai 2022 kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona.

Wakati Neville akijiandaa kuachia nafasi hiyo, Sarina amesaini mkataba wa miaka 4 kuiongoza timu ya taifa ya wanawake “Lionesses”. Mkurugenzi wa FA katika soka la Wanawake – Baroness Campell amesema ” Sarina alikuwa chaguo letu namba moja”.
Akizungumzia uteuzi huu, Sarina amesema ” England ni chimbuko la soka, ninajiandaa kuchangia uzoefu na utaalamu wangu katika timu hii yenye ari kubwa. Nilikuwa na wakati mzuri na kikosi cha Orange Lionesses (timu ya taifa ya Wanawake – Uholanzi), ni safari ambayo bado hatujafikia pale tunapotazamia kufika.”

“Nina shauku kubwa ya kukinoa kikosi cha England Lionesses, kwa sasa ninafanyia kazi kikosi cha Uholanzi. Nitajitahidi kadiri niwezavyo kuhakikisha tunaongeza kurasa nyingine katika safari yao kabla sijaanza kazi yangu mpya.”
Watu mbalimbali wamekua na maoni kuhusu uteuzi huu. Mkurugenzi Mkuu wa FA– Mark Bullingham amesema ” Sarina alikuwa na nafasi kubwa ya kuteuliwa, ni mshindi aliethibitishwa. Tunaamini ataisaidia England kufika mbali na kutupatia fursa ya kubeba makombe.”

Baroness Campbell amesema ” Sarina anaendana na utamaduni wetu, kitu ambacho ni muhimu sana katika kutengeneza timu.Uwezo wake wa kiufundi, uongozi na shauku ya kutaka ushindi ni vitu vikubwa sana.”
Kabla ya uteuzi huu, Sarina Wiegman amecheza michezo 104 na alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi. Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya wanawake ya ADO Den Haag na kisha akawa kocha msaidizi wa timu ya taifa mwaka 2014 kabla ya kutajwa kuwa kocha mkuu 2017.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Asia Abdy
Hongera kwake
Njiku
Hongera sana kwake ziende
Sadick
Soka la wanawake linakua siku hadi siku na kupata umaarufu na bila shaka uteuzi huu wa kocha unaendelea kuongeza mafanikio ya soka la wanawake#meridianbettz
Gabriel
Huyo n kocha mzur sana alishawai kuchukua tuzo ya kocha bora kwa upande wa wanawake mwaka 2017 ambapo wa kiume alikuwa zinade upande wang namtambua Kama kocha mzuri kwan Sarina Wiegman amecheza michezo 104 na alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi. Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya wanawake ya ADO Den Haag na kisha akawa kocha msaidizi wa timu ya taifa mwaka 2014 kabla ya kutajwa kuwa kocha mkuu 2017
Hivyo n habar njema sana timu ya wanawake England kupata kocha bora
Devotha
Hongera yake 👏👏wanawake tunaweza💪
Issa
Neville akuiwezea hii timu labd weigman sababu ni mchzaji wa kike
Furahav
Hongera kwake sarina.
Hope mwaikuka
Kila la heri kwake namkubal sana
Sabrina
Hongera sana
Fatuma kasomo
Safi
neema hassan
Pongezi kwake anastahil
Latifa juma mohamed
Hongera kwake sarina.
Theckla
Ni kocha mzuri na anajua majukumu yake
Johnmary joel
Hongera zake wanawake tunaweza zidi kupambana timu isongembele zaidi#Meridianbett
David Pere
soka la wanawake linakua siku hadi siku na kupata umaarufu na bila shaka uteuzi huu wa kocha unaendelea kuongeza mafanikio ya soka la wanawake hasa kwa wakati huu
Jibu
Gabriel
Omary lukumbi
Hongera sana sarina
Dorophina
Hongera kwake Sarina kwa kupata majukumu mapya timu za wanawake kwa sasa zinazidi kupanda chati
Mwanahamisi
Hongera kwake
aisha
Wanawake nao sasa ivi wamekua ni watu wanaojituma sana hivyo basi anasitahili kupata pongezi
Tatu
Pongezi kwake na raha sana kuona kila siku wanawake tunajitahidi kupanda kwenye uongozi
warda
Wamelamba Dodo Sarina bonge la kocha#Meridianbettz
Nasra
Sarina anastahili pongezi
Adelta
Hongera Sana kwake
@meridianbettz
Caroline
Ana uwezo mkubwa wa kuongoza timu
Mwajumah
Ongera yake anastahili
Mariam mtandama
Safi sana
Ernest
Profile ya Wiegman inaonyesha kuwa waingereza wamepata kocha Bora sana kwa upande wa wanawake naona tutarajie makubwa kutoka kwake, Kila la heri Wiegman
Sauda
Hongera kwake
Lydia Emmanuel Magoti
Pongezi kwake Wigman
felister
pongezi kwake wanawake wakiwezeshwa wanaweza
Shafii
Soka la wanawake kwa sasa limekua likifatiliwa na kupendwa duniani ni habari nzuri Sana.
Samira
Waingereza wamepata kocha bora sana kwa wanawake hongera wiegman
Fatina mfingi
Nice
Zeiyana
Ni jitiana kubwa sana alizo fanya sarina hadi kufika kuwa kocha mkuu ongela sana
Khadija
ongera sana kwan wanawake pia tunaweza
Rehema
Good
Povel
Gud information
Saupha mohamed
Safii
Salma ngende
Habari nzuri kwa shabiki wake
Ester jackson
Ni wakati wa wanawake kusonga mbele
Samiah
Safi
farida ahmadi
Pongezi Sana wigman
magdalena
pongezi kwake timu ya wanawake inazidi kupamba moto
Theonestina
Hongera yake