Beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold ametoka kimasomaso katika kinyang’aro cha tuzo ya mchezaji bora kijana wa msimu katika ligi ya Premier League.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga goli 4 na kuhusika kwenye magoli 13 zaidi katika msimu wenye mafaniko 2019-20 na kuona Liverpool wakinyanyua ndoo baada ya ukame wa miaka 30.

Alexander, Alexander-Arnold Anyakua Tuzo ya mchezaji bora kwa Vijana., MeridianbetTakwimu za Trent Alexander-Arnold msimu 2019-20

Alexander-Arnold pia alisaidia mabingwa hao kupata Clean sheet 12, na kuona mchezaji huyo akiibuka kinara kwenye kinyang’anyiro hicho na kuwabwaga wachezaji wa Manchester United Mason Greenwood, Anthony Mrtial na Marcus Rashford.

Wachezaji wa wili wa Chelsea pia walikuwepo kwenye kinyang’aro wachezaji hao ni Christian Pulisic na Mason Mount pia mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish na Dean Henderson wa Sheffield United walikuwepo.

Tuzo ilikuwa maalumu kwa wachezaji wenye umri wa miaka 23 au pungufu kwa msimu 2019-20 na kura zilipigwa na mashabiki.

Alexander-Arnold pia yupo kwenye ushindani wa mchezaji bora wa msimu kwenye Premier League, akiwa na mchezaji mwenzake Jordan Henderson na Sadio Mane lakini pia kuna Kevin De Bruyne, Jamie Vardy, Nick Pope na Danny Ings.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

soma zaidi

41 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa