Liverpool hawana mpango wa kumsajili kinda wa miaka 18 -Talles Magno kutoka Vasco da Gama ambaye amepewa jina la “Neymar wa Kesho”.

Tetesi kutoka katika vyanzo vya habari za michezo nchini Brazil zilitaja kuwa Liverpool wanataka kumsajili kinda huyu ambaye anatazamiwa kuja kuwa na uwezo kama wa Neymar kwa siku zijazo.

Kwa mujibu wa Evening Standard, Liverpool wameshafanya maamuzi juu ya kinda huyu na hawana mpango wa kumsajili kwa sasa.

Talles Magno -Next Neymar
Talles Magno -Next Neymar
Talles Magno alipata umaarufu kwa kuweza kuonesha uwezo wake katika kikosi cha vijana cha timu ya taifa ya Brazili U17, kwa kuchapa magoli 5 kati ya mechi 10 alizocheza na kuwasaidia kushinda Kombe la Dunia mwaka jana.

Hata hivyo, taarifa zinataja kuwa hofu kubwa ya Liverpool ni uwezo wa nyota huyu chipukizi kubadilisha mazingira ghafla, kutoka katika soka na utamaduni wa Brazil na kuendana na mahitaji ya soka na utamaduni wa Uingereza.

Magro ana mkataba na klabu ya Vasco da Gama hadi mwaka 2022, na mkataba wake unatajwa kuwa na thamani ya £43m. Lakini, kutokana na changamoto za janga la Corona klabu hii inatarajiwa kuwa inaweza kupokea hadi £18m.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

soma zaidi

44 MAONI

  1. Brazil kuna Neymar lukuki tatizo wakishaanza kupata umaarufu na fedha tabia hubadilika na kupoteza uwezo wa kucheza kabumbu. Kaka ni miongoni mwa wachache waliobaki na tabia njema maisha yao yote#meridianbettz

  2. Hapa wanahofia kwanza dau pili Kama watamsajir itabid akae bench kwanza ili wajue watampa namba gan maana dogo huyo Talles Magno anaonyesha kabisa n hatar sana 👍

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa