Gareth Bale yuko fiti kwa asilimia 100 na yuko tayari kwenda Kombe la Dunia akiichezea timu ya Taifa ya Wales baada ya kusumbuliwa na majeraha ambayo yalimuweka nje ya uwanja.

 

Bale Yupo Fiti na Tayari kwa Kombe la Dunia

Winga huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa na wasiwasi kabla ya Robert Page kutaja kikosi chake cha wachezaji 26 kwa mechi ya kwanza ya Wales kwenye Kombe la Dunia baada ya miaka 64.

Bale ameanza mara mbili pekee katika klabu ya Los Angeles FC tangu ajiunge nayo akitokea Madrid mwezi Julai, lakini alifunga bao la kusawazisha dakika za nyongeza  akitokea benchi walipokuwa wakicheza  dhidi ya Philadelphia Union kwenye fainali ya Kombe la MLS, ambayo LAFC ilishinda kwa penalti mnamo Novemba 5.

Awali Bale aliwapa Wales sababu ya kuwa na wasiwasi baada ya fainali hiyo kwani alisema anahisi hatoweza kucheza kwa 100% lakini tangu wakati huo amekuwa fiti na yupo tayari kulipambania Taifa lake.

Bale Yupo Fiti na Tayari kwa Kombe la Dunia

Bale ameiambia Sky Sports kuwa; “Niko fiti kwa asilimia 100 na niko tayari kuondoka, na ninadhani kwa kila mtu wiki tatu au nne zilizopita, imekuwa ngumu hata kusikia hadithi za wachezaji kushuka na kujua watakosa Kombe la Dunia”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa