Mchezaji wa PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi anaona ufanano kati ya timu hii ya Argentina na ile ambayo ilikosa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka wa 2014.

 

Messi Afananisha Kikosi cha Argentina na Kile Cha 2014

Argentina itaelekea Qatar mwezi huu ikitafuta kunyanyua kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu 1986.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, ​​Messi, ambaye sasa anachezea klabu ya Paris Saint-Germain inayomilikiwa na Qatar, amesema huenda likawa Kombe lake la mwisho la Dunia kucheza mwaka huu.

Bado hajashinda tuzo kubwa zaidi katika soka ya Kimataifa, ingawa aliisaidia La Albiceleste kutwaa taji la Copa America mwaka 2021 baada ya kuifunga Brazil, huku  akimaliza kama mfungaji bora akiwa na mabao nane.

Messi Afananisha Kikosi cha Argentina na Kile Cha 2014

Messi alishinda Mpira wa Dhahabu mwaka wa 2014 baada ya kuiwezesha Argentina kutinga fainali, na kubaki tu kutazama Ujerumani ikisherehekea kufuatia Mario Gotze aliyefunga bao la dakika za nyongeza.

Lakini, akizungumza kabla ya mashindano ya 2022, Messi alionekana kupendekeza kikosi hiki cha Argentina kina umoja wa kufikia timu ya 2014, akisema kuwa; “Katika Kombe la Dunia la 2014, tulifanya vyema sana na ilikuwa ni uzoefu usiosahaulika”

Aliendelea kusema kuwa alifurahi sana na kwamba jambo kuu na muhimu zaidi ni kuwa kikundi chenye nguvu na umoja. Na hatimaye anahisi kufanana sana kati ya kundi hili la Argentina na lile la 2014.

Messi Afananisha Kikosi cha Argentina na Kile Cha 2014

Argentina imekuwa ya pili  kupendwa nyuma ya wapinzani wao Brazil kushinda Kombe la Dunia la 2022, huku vijana wa Lionel Scaloni hajapoteza tangu walipochapwa 2-0 Copa America na Brazil katika Fainali ya Copa America 2019, mfululizo wa michezo 35 bila kupoteza

Argentina Wanaanza kampeni ya Kombe la Dunia dhidi ya Saudi Arabia mnamo Novemba 22, kabla ya kumenyana na Mexico na Poland katika mechi zao nyingine za Kundi C.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa