Young: Ilikuwa Rahisi Kujiunga Inter

Baada ya kudumu kwenye kikosi cha Manchester United kwa miaka 8. Ashley Young aliamua kujiunga na Inter Millan mapema mwezi Januari.

Young ambaye alikuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Manchester United. Alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya Ole Gunnar Solskjaer kukabidhiwa mikoba ya Mourinho.

Young
Ashley Young akishangilia ushindi wa Man United

Ujio wa Solskjaer ulileta neema kwa wachezaji vijana huku wachezaji wenye umri mkubwa wakitumika mara chache sana. Young (35) alijikuta kwenye wakati mgumu zaidi baada ya ujio wa Aaron Wan Bissaka na kuchipukia kwa Brandon William, nafasi za vijana hawa zilimfanya Young kukosa namba kwenye kikosi cha Manchester United.

Akizungumzia suala hilo wakati alipofanya mahojiano na ukurasa wa Uefa, Young amenukuliwa akisema, ” Kuwepo kwangu England maisha yangu yote, kiukweli yalikua ni mabadiliko makubwa. Ilikuwa ni fursa yangu ya kwenda kucheza mara kwa mara.”

Young
Ole Gunnar Solskjaer akifurahi na Ashley Young

” Nilizungumza na Ole na alinambia sitokuwa nikicheza mara kwa mara kama nilivyokuwa ninahitaji. Ukiwa unaelekea mwishoni mwa muda wako wa kucheza soka, unahitaji kuwa unacheza mara kwa mara. Nipo vizuri kama wachezaji wengine na bado ninavitu vingi vya kuonesha.

“Kwa upande wangu umri ni namba tu. Ole alisema atawapa nafasi wachezaji vijana na hivyo sitokuwa na nafasi kubwa. Fursa ya kujiunga na Inter ilipokuja, ilikuwa ni jambo rahisi kwangu. Nilihitaji kupanda ndege na kuondoka eneo lile [Man United] mapema kabisa.

Young
Romelu Lukaku na Ashley Young

“Nilikuwa nikizungumza na kocha pamoja na wachezaji wa hapa [Inter Millan] niliokuwa ninawafahamu. Ilikuwa ni fursa nzuri, moja ya klabu kubwa duniani katika ulimwengu wa soka.”

Katika kuelekea mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Shaktar Donetsk, Young amezungumzia namna ya ufundishaji wa kocha wake – Antonio Conte.

Conte anahitaji kila kitu, sio uwanjani tu hata kwenye mazoezi. Unaweza kusema ni mshindi, anahitaji ushindi na anataka hilo litimizwe na kila mchezaji. Kila mmoja ana akili ya ushindi.

Young
Kocha wa Inter Millan – Antonio Conte

Serie A ni ligi inayotumia sana mbinu kuliko nilivyokuwa nimezoea, lakini ni moja ya vitu unapaswa kuvizoea na ninadhani nimeshazoea. Kucheza kama winga mkabaji kunahitaji mbio nyingi na kushambulia, ni vitu ambavyo nimevizoea na imenisaidia kufunga magoli na kutoa pasi za magoli.

“Nilipokuwa Man United, nilikuwa kama mlinzi zaidi. Ukiwa hapa [Inter] unapaswa kuwa unashambulia zaidi kuliko kukaba.”

Young

Akiwa Manchester United, Young alibeba makombe 5 likiwemo ya Ligi Kuu Uingereza- EPL. Pia, alikabidhiwa unahodha wa timu hiyo baada ya Antonio Valencia kuondoka Old Trafford. Inter Millan walimsajili kwa ada ya euro milioni 1.5 kabla hakuwa mchezaji huru.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

39 Komentara

    Young hakua mbaya ila umri aliokua nao na mara nyingi alikua anatoa boko sana

    Jibu

    Habari njema sana

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Habari njema kwetu

    Jibu

    Meridianbet mpo vizur!!!!

    Jibu

    Maoni:hata ivyo inter sio timu ndogo

    Jibu

    Sawa

    Jibu

    Habari njema sana#Meridianbettz

    Jibu

    Habari njema hizi

    Jibu

    Young Yuko vizuri
    @meridianbettz

    Jibu

    Ashley young alisumbua sana kipindi kile alivyo kua man Chester utd..!kwa mri alio kua nao sasa hivi me sioni kama hamefikia mri mkubwa hadi kufikia yeye kuona so wanapo ingia wachezaji chipukizi kikubwa angalie tu kuna mchezaji amabaye hanayeweza kufikia kiwango chake

    Jibu

    Young ni mchezaji mzuri sana basi tuu muda wake ukifika asijali nyota yake itang,ara

    Jibu

    Sawa

    Jibu

    Mpo juu meridianbet

    Jibu

    Bado young anadai kabisa hakipangwa kikosoni bora alivyoenda inter

    Jibu

    Young Hana shida mbona

    Jibu

    Mpo vizuri kwa taarifa

    Jibu

    Yaung yupo vizuri

    Jibu

    Hapo ndio panakufaa kijana

    Jibu

    even if inter sio timu mbaya

    Jibu

    Shughuli ya Young wanaijuwa huko Italia, Amekuwa msaada mkubwa sana kwa Inter

    Jibu

    Safii sana young we kipute inter waache man u wakigwaya gwaya na timu lao bovu lisilo LA ushindani

    Jibu

    Kweli umri ni namba tu kama alivyosema mwenyewe Ashley Young kwa maana siku za karibuni amekuwa moto wa kuotea mbali pamoja na umri wake kuwa mkubwa. Niliona akifunga magoli mawil kwenye mechi ya Inter dhidi ya mshindi wa tatu ktk Ligi Atalanta#meridianbettz

    Jibu

    Italy ndo inchi ambayo inawatumia Sana wakongwe kwenye soka la miguu.

    Jibu

    Kijana anajua

    Jibu

    Kwa tunavyo faham ligi ya inter awaangaliagi umri isipo kua uwezo ukiruhusu unacheza.

    Jibu

    Young amekuw kwenye kiwango bora toka atue inter

    Jibu

    Inter wanaangalia uwezo wa mtu

    Jibu

    Habari nae.

    Jibu

    Young ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Namkubali sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Safii sana young we kipute inter waache man u wakigwaya gwaya na timu lao bovu lisilo

    Jibu

    Safii Sana Ashley Young

    Jibu

    Kapotea huyu kwenye Gemu#Meridianbettz

    Jibu

    young yupo sahihi juu ya alisemalo bado yupo vizuri katika soka

    Jibu

    Young yuko vzur sana namkubal

    Jibu

    Serie A hua wanaangalia uwezo wa mchezaji sio umri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.