Baada ya kuonesha matamanio ya kuongeza uwezo wake kunako soka la Ulaya. Hatimaye Gabriel Magalhaes ameruhusiwa kuondoka Lille.
Inasemakana uwezekano wa beki huyo kucheza kunako Ligi Kuu Uingereza – EPL ni mkubwa kufuatia vilabu kama Manchester United na Arsenal kuhitaji saini ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 22, raia wa Brazil.
Akizungumza na BBC World Service’s World Football, mmiliki wa Lille – Gerard Lopez amesema, “Jinsi tunavyofanya kazi ni rahisi. Tumemuelezea [Gabriel] yeye na wakala wake kile tunachokihitaji, endapo kitatimizwa basi maamuzi yatakuwa ni yake. Kama tulivyofanya kwa Nicolas [Pepe] na Victor [Osmihen].

“Tumefikia hapo na tumemwambia, unapaswa kufanya maamuzi lakini hatukulazimishi. Nadhani ataamua wiki hii au mapema wiki ijayo. Anaondoka, tumeruhusu hilo.
“Kunaushindani mkubwa, bado ni mchezaji kijana. Anapaswa kufanya maamuzi yaliyosahihi. Tumemsaidia kidogo hivyo tumemwambia, tunadhani huyu ni kocha sahihi au hii ni klabu sahihi kwako. Anakipaji kikubwa, atafanikiwa popote atakapokwenda.”
Mapema mwezi Juni, Gabriel alikaribisha fursa za kujiunga na timu zingine alipoweka wazi adhima yake ya kutaka kuboresha zaidi kiwango chake.

Akizungumza na L’Equipe. Gabriel alinukuliwa akisema, “Ninahitaji kwenda mbali zaidi kadiri iwezekanavyo, nilikuja ulaya kwa ajili hiyo. Uingereza au Italia? zote ni sehemu zenye mashindano mazuri.
“Popote nitakapokwenda, nitaweza kucheza katika nafasi ya juu. Kikubwa zaidi ni katika timu itakayoniruhusu kucheza kwa nafasi.”

Lille wapotayari kumuuza Gabriel kwa timu yeyote itakayowalipa pauni milioni 25. Inafahamika kwamba kocha wa Man United – Ole Gunnar Solskjaer yupo sokoni kumtafuta beki wa kati anayetumia mguu wa kushoto atakayecheza na Harry Maguire msimu ujao.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Omary lukumbi
United chukua jembe hilo
Ester jackson
Good news
Angelina
Goodupdate
Venerose
Asante kwa taarifa
Rose kapinga
Maisha popote angalia maslahi yako!!!
Theonestina
Kazi kwake kuchagua wapi pa kwenda
rama
Maoni:vizuri aje EPL
Mwajumah
United chukua jembe ilo ni noma sana#Meridianbettz
aisha
Uamuzi ni wako uende unapotaka
Dorophina
Itakuwa poa kama Gabriel akienda kwa mashetani wekundu
Adelta
Manchester chukueni jembe Hilo
Bado kijana mbichi kabisa@meridianbettz
Zeiyana
Akienda arsenal itakua vizuri kwa uwezo alio kua nao Gabriel ndio kutamfaa zaidi na sio man Chester
Sabrina
Hapo inabodo Arteta achangamke amchukue Gabriel ilikipanga kikosi cha Arsenal vizuri
Mwanahamisi
Kambi popote ni bora haangalie maslahi yake
Fatina mfingi
Makala nzur
Caroline
Asanteni kwa taarifa
Sauda
Kambi popote, Cha muhimu mkwanja tu..
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri alicho kiamua kambi popote
Tatu
Naisi atachukuliwa man
felister
kikubwa maslai
Ernest
Juhudi za Gabriel Magalhaes zitazaa matunda muda sio mrefu, Kila la heri Gabriel Magalhaes
Njiku
Man wanatakiwa wasajili ili kuendana farsafa ya soko waache uingereza mwingi
Sadick
Nadhani mahali sahihi kwa Gabriel ambapo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara ni Chelsea#meridianbettz
Nasra
Maamudhi Ni yake na siku zote wachezaji hua Wana ndoto zao katika career ya mpira na Gabriel nadhani anaona sio sehemu sahihi lile ya kutimiza ndoto zake.
Saupha mohamed
Maslai ndokila kitu
Samiah
Maslai ndokila kitu
Shafii
Ndoto zake anahisi haziwezi kutimia akiwa na Lille.
Issa
Epl ndio ligi ya ushindani gabriel kaonyeshe uwezo
Janeflora malisa
Uwamuz mzr
Furahav
Njoo man u
Devotha
Aende arsenal
Hope mwaikuka
Taarifa imeeleweka
Povel
Maisha popote kila la kheri
David Pere
Juhudi za Gabriel Magalhaes zitazaa matunda muda sio mrefu, Kila la heri Gabriel Magalhaes kapige boli dogo
Latifa juma mohamed
Maisha popote kila la kher
farida ahmadi
Kambi popote
warda
Hatumtaki sie Man U #Meridianbettz
magdalena
itapendeza zaidi gabriel akitua united
Gabriel
Hatimaye Gabriel Magalhaes ameruhusiwa kuondoka Lille n habar njema matumain yang aje ata arsenal maaana kwa kiwango chake anatakiwa kupata timu yenye mfumo mzur wa uchezaji coz haina ya uchezaji wake utampendeza akiingia Arsenal
Shan
Maamuzi anayo mwenyewe kubaki au kuondoka.