Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amefunguliwa mashitka na chama cha soka cha nchini Uingereza FA kwa kwa kuupa mchezo sifa mbaya baada ya kudai kuwa Liverpool walipata faida ya upendeleo kwa mwamuzi wa mchezo huo kwenye dimba la Anfield.

Frank Lampard alitia neno baada ya ya timu yake kupokea kichapo cha 2-0 dhidi ya wapinzani wake mwezi uliopita, heshima kwa magoli ya Andy Robertson na Divock Origi waliyoyafunga kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo.

Frank Lampard

Kwenye mchezo huo Anthony Gordon alifanyiwa madhambi na mlinzi wa klabu ya Liverpool, Joel Matip kwenye eneo la hatari lakini mwamuzi hakuweza kuwazadia penati hata walipoombwa waamuzi wa VAR na walisema sio penati, hilo ndio tukio ambalo Frank Lampard amekuwa akililalamikia zaidi.

“Frank Lampard ameshitakiwa kwa kuvunja kanuni ya E3 ya FA ikihusu matamko yake kwenye vyombo vya habari baada ya mchezo ambayo aliitoa kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Liverpool siku ya jumapili 4 April 2022, ikisomeka.

“Ni kosa kwa kocha kutoa kauli za shutuma zisizo faa kama upendeleo au kumshamburia mwamuzi wa mchezo kuhusu uaminifu wake au waamuzi wote kwa ujumla na kuleta  sifa mbaya ya mchezo na kulingana na kanuni ya E3.1. lampard hadi siku ya jumatatu awe amewasilisha majibu 9 May 2022.” Waraka wa FA.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa