Nyota wa Real Madrid anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich ameanza kuwashughulisha wakubwa wengi barani Ulaya ikiwemo Uingereza kuanza kuhitaji huduma yake msimu ujao japo nyota huyo anapendelea kusalia ndani ya jiji hilo na kuendelea kucheza huko lakini klabu kama Liverpool, Manchester United na Arsenal zimeanza kufukuzia huduma yake ili aweze kutua katika jiji hilo.
Asensio hauzwi, matajiri wa jiji la Hispania, klabu ya Real Madrid wamebainisha kwamba nyota wao wa klabu hiyo, Asensio hawezi kuingia sokoni kwa sababu bado wana matumizi naye na bado kikosi chao kinamhitaji sana. Hii ni baada ya Spurs kuanza kujishughulisha kumhitaji nyota huyo lakini klabu haipo tayari kumtoa nyota huyo ambaye kwa hakika ndicho kizazi cha Madrid mpya.
Sane awavutia Bayern, je, ni kweli kwamba watakubaliana nyota huyo kupisha milango ya wengine au watakomaa na walichonacho badala ya kutumia fungu jingine la pesa? Klabu hiyo kwa sasa ipo njia panda kama imuuze Sane ambaye anapiganiwa na Bayern ili waingie sokoni kupambana na United kuwania saini ya fundi wa Benfica, Joao Felix ambaye amekuwa na msimu wa pekee sana ndani ya kikosi hiyo.
Delph naye sokoni, mchezaji wa City ambaye hajaonekana sana uwanjani msimu huu ametengewa kiasi cha £15m. Kwa klabu yoyote itakayokuwa tayari kulipa kiwango hicho City watakuwa tayari kumuachia nyota wao huyo ili kupunguza idadi kubwa ya wachezaji na kupata maingizo mapya ili kuleta ushindani zaidi. Sio hilo pekee pia, hajawa na msimu wa kiushindani sana ndani ya kikosi hicho.
Perisic na pesa juu, Inter Milan wanaonekana wanamaanisha kweli katika biashara yao baada ya kuwaonesha United kwamba wanamhitaji nyota huyo na wapo tayari kuongeza kiwango fulani cha fedha ili kumnasa nyota huyo. Wametenga kiasi cha £30m na watakuwa tayari kumtoa Perisic awe kama mbadala wa nyota huyo raia wa Ubelgiji. Hajawa na ushindani sana ndani ya kikosi cha United lakini anashawishi sana sokoni.
United mbioni kuwanasa Rabiot na De Ligt, klabu hiyo kwa sasa ina maeneo mengi inahitaji ikiwemo ulinzi, kiungo na ushambuliaji hivyo wanaona kwamba kusajili nyota hawa inaweza kuwa na nguvu fulani ndani ya kikosi chao ambacho hakijawa vizuri kwa msimu mzima. Wanahitaji wachezaji wa kutosha na wenye takwimu za juu ili kupisha aibu hiyo isijirudie upya misimu ijayo.


aisha
Hongera sana mmefanya vizuri