Kwanini Washinde Euro 2020?

Baada ya kuanza vyema katika kampeni yao ya kufuzu kuelekea kwenye michuano ya Euro 2020 kwa kushinda mechi zao mbili; vijana wa Southgate wanapigiwa chapuo kuipeperusha bendera ya taifa la Uingereza vyema kabisa. Kikosi hicho kilifanya vizuri sana kwenye michuano ya kombe la dunia kule Urusi kwa kufika hatua ya nusu fainali.

Japo bado wana kibarua kizito sana kuwaaminisha mashabiki zao kuhusu nafasi yao hiyo kutokana na kuwa wahanga wa ukame wa makombe ndani ya kikosi chao. Jambo hilo bado litakuwa msamiati kwa Southgate. Kuna vitu vinawapa nafasi kubwa sana ya kutwaa kombe la michuano ya Euro 2020 kama vile:

Euro 2020 itakuwa ndani ya ardhi yao, michezo mingi sana inategemewa kufanywa katika uwanja wake wa Wembley na hiyo ni faida kwake kwa sababu atakuwa na mashabiki wengi ambao watampa nguvu kubwa ili kumthibitishia nafasi kubwa akiwa nyumbani. Watakuwa wakikumbuka historia hiyo ya mwaka 1996 walipoandaa michuano hiyo na kuishia kupigwa na Ujerumani kwenye mikwaju ya penati.

Wana kikosi chenye wachezaji wazuri, ni jambo lislofichika kwamba kizazi cha Uingereza kwa miaka ya hivi karibuni kimekuwa sana na kimezalisha wachezaji wenye uwezo wa pekee sana. Uwepo wa majina kama Harry Kane, Raheem Sterling, Marcus Rashford, na Jesse Lingard kwa hakika ni mbegu kubwa ilipandwa. Mbali na hao kuna watu kama Jadon Sancho, Callum Hudson-Odoi, Kyle Walker, Trent Alexander-Arnold na Kieran Trippier, Danny Rose, Ben Chilwell, Luke Shaw, Jordan Henderson, Declan Rice, Harry Winks, Ross Barkley ambao hakika hawashikiki kabisa.

Wachezaji wengi bado vijana lakini tayari wamezoea ushindani, ni kizazi endelevu chenye vijana wengi ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakishiriki ligi kubwa barani Ulaya ambazo ushindani wake ni mkubwa sana kitu ambacho kinawapa asilimia kadhaa kuwa kidedea. Idadi kubwa ya wachezaji umri wao unahesabu kwenye miaka 20 hadi 25 na wachache sana wamefikisha 29. Wakongwe ni wachezaji kama Henderson.

Kikosi kinachoonekana kuleta ushindani kwao ni Ufaransa pekee.

Mafanikio waliyoyapata kwenye kombe la dunia kufikia hatua ya nusu fainali ni kitu ambacho kwa hakika kimewajengea heshima na kuonesha kwamba wana uwezo mkubwa sana. Nguvu waliyoitumia kufikia hatua ile pia itaonekana katika Euro 2020 kwa sababu bado hakijaharibika kitu wala kupungua kitu ndani ya kikosi chao.

Matumizi ya mifumo yake ya 3-5-2 na 4-3-3 ni nguzo kubwa ambayo imempa matokeo mengi na ataendelea kuitumia hiyo kutokana na wachezaji alionao kocha wao.

Makala iliyopita

2 Komentara

    England ni moja kati ya Mataifa yenye wachezaji wazuri na ligi yao ya kuvutia,nina imani watafika hatua za juu kwenye EURO

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.