Gabriel Kuchagua Kati ya Arsenal na Napoli

Mlinzi wa LilleGabriel Magalhaes anategemewa kuchagua timu atakayoitumikia kuanzia msimu wa 2020/21 ambapo mpaka sasa ni timu 2 – Arsenal na Napoli ndio zimewasilisha ofa zao za usajili.

Baada ya kuwa na msimu mzuri kunako Ligue 1, nyota imemuwakia Gabriel na sasa uwezekano wa kucheza EPL au Serie A upo mikononi mwake. Taarifa za chini chini zinasema uwezekano wa kwenda Arsenal ni mkubwa kuliko Napoli.

Akizungumza na talkSPORT baada ya kuulizwa kuhusu ofa ya Arsenal, Napoli na Manchester United, Raisi wa Lille – Lopez amesema ” kunahizo na nyingine nyingi.Nadhani amezipunguza.

“Nadhani ni sahihi tukisema Arsenal wameonesha nia zaidi, Napoli pia.

“Tumempatia muda wa  kutosha kufanya maamuzi. Tumekuwa tukisema kila mara ‘kama tukiwa na makubaliano sawa na timu 2 au 3, basi hatutokuwa na ushindani wa ofa’.

“Na huo ni uamuzi, sidhani kama ninakata tamaa mapema nikisema huo uamuzi ni leo au kesho. Nashindwa kuwaambia uamuzi huo ni upi. Tumempatia mapendekezo kadhaa lakini hatutaki kuyasema hadharani, hatutaki kumfanya mtu ajisikie vibaya.

Je, Gabriel Ataenda Arsenal au Napoli?

“Tumezungumza kuhusu wapi anapaswa kwenda, lakini  mwisho wa siku ni yeye na mazingira yake ndio vitaamua na tutakubaliana na hilo.”

Inasemekana Lille wamepokea ofa ya takribani euro milioni 24 na wanategemea Gabriel atafanya maamuzi sahihi ndani ya muda mfupi na mpaka sasa hayupo kwenye kikosi cha Lille kinachojiandaa na msimu ujao.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

36 Komentara

    Wahenge walisemah kipendacho roho hura nyama ndichi ngoj tuone fundiiii wa mpr Gabriel atachagua chama gan gunners au Napoli

    Jibu

    Uamuzi ni wake

    Jibu

    Uhamuzi anao yeye ,na vilevile hatskuwa amepiga hatua kwenda sehemu nyingine anakuwa anaongezea na ujuzi zaidi kujifunza zaidi

    Jibu

    Maamuzi yake

    Jibu

    Gabriel aende Arsanal bhana

    Jibu

    Uwamuz ni wake

    Jibu

    Hata wa kale walinena kila ndege hutua mti aupendao, lakini mwisho wa siku ni yeye na mazingira yake nyota Gabriel ndio vitaamua na tutakubaliana na hilo.”

    Jibu

    Na huo ni uamuzi, sidhani kama ninakata tamaa mapema nikisema huo uamuzi ni leo au kesho. Nashindwa kuwaambia uamuzi huo ni upi. Tumempatia mapendekezo kadhaa lakini hatutaki kuyasema hadharani, hatutaki kumfanya mtu ajisikie vibaya.

    Jibu

    Uamuzi ni wake

    Jibu

    Uamuzi anao yeye

    Jibu

    Mahamuzi ni yake!

    Jibu

    Aende tu Napoli#Meridianbettz

    Jibu

    Uingereza inaaminika soka lake linamvuto sana lakini binafsi sijaona bado, Kwa hoja hii moja kwa moja kijana Gabriel atachagua Arsenal

    Jibu

    Ni uamuzi wake tu

    Jibu

    Aende arsenal mana ni timu kubwa histoshe kama atafanya vizuri kwenye klabu hiyo anaweza kwenda timu kubwa zaidi ila maamuzi ni yake

    Jibu

    Maoni:nivyema akaenda kukipiga EPL

    Jibu

    Uwamuzi ni wake

    Jibu

    Gabriel chaguo lipo kwake wapi haende ila kwa mtazamo wangu kama arsenal patamfaa

    Jibu

    Gabriel lazima ataenda arsenal

    Jibu

    Uamuzi ni wake

    Jibu

    Maamuzi Ni yake
    @meridianbettz

    Jibu

    Arsenal ndio kutamfaa zaidi.ila yeye mwenyew ndio hana maamuzi yake

    Jibu

    aende arsenal patamfaa zaidi

    Jibu

    Uwamuzi niwake anapo pendekeza yeye kwenda ndio atapo kwenda yeye anajua anacho kifanya kwenye akili yake

    Jibu

    Gabriel mwenyewe ndio atachagua pa kwenda msimu huu

    Jibu

    Gabriel mwenyewe ndio atachagua mahali wapi patamfaa ila bora aende arsenal

    Jibu

    Mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama, hapa Arsenal wanaonyesha kuwa na kisu kikali zaidi watia nia wote#meridianbettz

    Jibu

    EPL ndo ligi pendwa dunian me sidhan kama Kuna chaguo hapo zaid ya arsenal

    Jibu

    Mmh

    Jibu

    As long as its ok to him

    Jibu

    Aende tu Arsenal.

    Jibu

    Napoli ndio sehemu ya kukuza soka lako

    Jibu

    Mmi ningemshauri atimkie arsenal atapata nafasi ya kucheza.

    Jibu

    Aende napoli

    Jibu

    Uamuzi ni wa kwake yeye mwenyewe

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.