Gareth Bale tayari anaripotiwa kuwa amekubali kuhama kabla ya kumalizika kwa mkataba wake Real Madrid.

Mchezaji huyo wa Wales amekuwa na wakati mgumu kwa kukosa muda wa kutosha wa kucheza Real Madrid msimu huu tangu kurejea baada ya kucheza kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Tottenham msimu uliopita.

Ingawa, sehemu kubwa ya kutokuwepo kwa Gareth Bale kumetokana na majeraha, huku  akirejea baada ya changamoto iliyomsumbua kwa karibu wiki mbili zilizopita au zaidi.

Tottenham Hawana Shida Tena na Gareth Bale
Gareth Bale Anatarajia Kurejea Tottenham kwa mara ya tatu.

Baada ya kucheza mechi tatu mwanzoni mwa msimu, Bale alikaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na tatizo la mgongo. Amerejea hivi karibuni lakini ameachwa benchi na Carlo Ancelotti.

Gareth Bale bado anaweza kucheza katika miezi ijayo, lakini ni hakika kwamba mkataba wake, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hautaongezwa tena.

Na kwa mujibu wa El Nacional, mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales tayari amekubali kusaini mkataba wa awali na Tottenham.

Inadaiwa Bale atarejea Spurs kwa mara ya tatu ukiwa ni mkataba wa mwisho wa maisha yake ya soka. Ripoti hiyo inadai Bale alikubali mpango huo miezi mitatu iliyopita.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa