Grealish, Villa Wanamtaka, City Wanamnyemelea.

Nahodha wa Aston Villa, Jack Grealish awaeka kati Villa na Man City. Ni dhahiri kuwa Grealish ni muhimili wa Villa, lakini £100M za City zinaweza kuleta madhara.

Aston Villa imeshaanza mazungumzo ya kuboresha mkataba wa Grealish ambapo kwa sasa, mchezaji huyo yupo na Timu ya Taifa ya Uingereza hivyo mazungumzo yanayoendelea yanasimamiwa na wakala wake.

Nahodha huyu wa Villa anamkataba na timu hiyo mpaka 2025 na kama klabu, haina mpango wa kumuachia Jack muda wowote kwa siku za karibuni. Kocha, Dean Smith anamuhusudu mchezaji huyo na imeripotiwa mchakato wa usajili unaoendelea klabuni hapo, unalenga kuwaleta wachezaji wanaoweza kucheza na Jack kama muhimili mkuu wa klabu hiyo.

Pep Guardiola.

Japokuwa Pep Guardiola ni shabiki mkubwa wa Grealish, inaaminika kuwa Harry Kane na Erling Haaland ndio vipaumbele vya timu hiyo kwenye dirisha hili la usajili. Hii haimaanishi City hawana mpango na Jack la hasha! Kuna £100M ambazo zimeripotiwa kutolewa na City kama dau la kumsajili nahodha wa Villa.

Ni uhalisia usiopingika kuwa City watapaswa kuuza wachezaji kabla ya kusajili mchezaji wa gharama kati ya Kane, Haaland na Grealish mwenyewe.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe