Henderson Kupewa Kipa No. 1 United?

Mchezo wa jana kati ya Man United na Spurs ulionesha uwezo mkubwa wa kipa namba mbili wa United Dean Henderson. Henderson amekuwa akitumika katika mechi za aina fulani kwa Manchester United huku Kipa anaaminika kuwa namba moja wa United, Muhispania David De Gea akikaa benchi.

Kwa muda sasa Ole hajataka kuweka wazi kipa wake namba moja tu yupi. Lakini kutokana na kucheza vizuri kwa Henderson, wachambuzi wakubwa duniani wa soka wanaamini kwamba huu ni wakati sahihi kwa Henderson kuwa namba moja wa United.

Katika mechi ya jana, Dean alionekana kuwa mtulivu na kujiamini sana licha ya ukubwa wa timu Tottenham. Dean alifanikiwa kuokoa michomo kadhaa ya moja kwa moja na ile ya mbili.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, ambapo mashetani hao wekundu walipokea kichapo cha 6-1, David De Gea alikuwa langoni. Lakini jana Dean Henderson akiwa golini Man united waliruhusu goli moja tu! Katika mechi hiyo hiyo Manchester waliyopoteza, Ukuta wa United ulikuwa chini ya Nahodha Harry Maguire na Eric Baily ambaye yeye pia alikosa mchezo wa jana.

Tottenham pia walitangaza nia ya kutaka kupata huduma ya kipa huyu kinda wa Man United, je, Dean anaweza salia United kama kipa namba moja au akaondoka na kutimka kwingineko?


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Hongera yake

    Jibu

    Dean Henderson yuko vizuri

    Jibu

    Dean ni kila bora

    Jibu

    Vzur

    Jibu

    Sio mbaya mana degea tumekaa nae sana

    Jibu

Acha ujumbe