CAF Kuleta VAR Robo Fainali Ya Ligi Mabingwa

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa taarifa kwamba litatembelea viwanja nane vitavyotumika katika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika ili kuangalia uwezekano wa kutumia usaidizi wa uamuzi wa video,VAR.

Ratiba ya robo fainali inategemewa kutoka tarehe 30 mwezi huu na tayari maofisa wa CAF wameahidi kufika viwanja vyote nane. Uwanja wa Benjamin Mkapa ni miongoni mwa viwanja hivyo, ambapo utatumika na Simba Sc kama uwanja wa nyumbani.

Kwa kawaida VAR hutumika katika mechi ya fainali tu, lakini inaonekana CAF wameamua kushusha mpaka robo fainali kutokana na matatizo au mapungufu mbalimbali yanayoonekana na waamuzi kwenye ngazi za awali za mashindano hayo.

Endapo suala hili litafanikiwa, itakuwa ni mwanzo wa maendeleo makubwa ya soka barani Afrika, kutokana na ukweli kwamba VAR imekuwa ikitumika katika kutatua maamuzi magumu.

Japokuwa bado kwa kiwango fulani VAR imekuwa ikigubikwa na mapungufu makubwa sana hasa kwenye kutoa penati na kutokuruhusu magoli, bado kwa sehemu kubwa mashabiki wanaamini kwamba VAR itasaidia kuleta mabadiliko kwenye soka la Afrika ambalo lina waamuzi wenye upungufu mkubwa sana.

Ni kosa gani ambalo mwamuzi wa bongo amewahi fanya ukatamani kungekuwa na VAR?


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

4 Komentara

    Ni Jambo zuri

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Ww

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.