Henry, Mwambie Aubameyang Apokee Simu Yangu au Ajifunze Kupitia Wewe

Hadithi nzima inaanzia ile jioni ya Agosti 3 mwaka 1999, waingereza walisimama kwa butwaa kubwa sana mitaa ya Longford London kumshangaa kijana mmoja mdogo sana aliyekuwa akiongozana na Arsene Wenger kuelekea maeneo ya Holloway yalipo makao makuu ya club ya Arsenal.

Mashabiki wengi wa Arsenal walihuzunishwa na usajili ule wakiamini Thierry Henry hakuwa na hadhi ya kucheza Arsenal, ila Wenger aliamua tu kumbeba kwa sababu alikuwa mfaransa mwenzake. Mitaa haikuwa inampa uzito sana. Wengi Jioni ile, walikuwa bize na ujio wa Davor Suker kutoka Real Madrid.

Walitazamana tu wakiambiana, “Si amefeli Juventus huyu mtoto? Jamani, kwani Arsenal ina shida winga? Hawa wafaransa wanabebana sana hawa.” Ila Wenger alimnong’oneza kwa kifaransa kijana wake ‘c’est la vie’ akimaanisha ‘ndiyo maisha jikaze.’

Ila laiti kama waingereza wangejua kuwa mzee Wenger kaleta ‘moto kama wa Sodoma’ kwa mabeki na makipa, wasingesema hovyo ile siku. Wenger alimuhamisha Henry kutoka eneo ka winga na kumfanya mshambuliaji wa kati. Kila mtu anajua nini kilifuata baada ya hapo.

Miaka nane aliyocheza Arsenal amepiga mabao 228, 175 yakiwa ya ligi. Mpaka kesho anabaki kuwa mfungaji wao bora wa muda wote. Amechukua mataji manne pale. Ameondoka na kiatu cha mfungaji bora wa msimu mara nne na amekuwa mchezaji bora wa mwaka mara tatu. Aliikosakosa ballon d’or ya 2003. Henry mtu bwana🙌.

Maisha yalienda kasi na Arsenal ilivurugika, ikapoteza ule uimara wake. Henry alivumilia kwa kuwa alipendana sana na Arsenal. Zaidi ya yote alimuheshimu sana Wenger. Ila Siku moja ya mwaka 2007 uzalendo ulimshinda. Henry akamfuata Wenger mazoezini na kumuambia. “Tuna timu nzuri sana ya vijana, ila najua hatuwezi kuchukua taji la ligi kwa sasa. Nina miaka 31, siwezi kusubiri vijana wakomae. Naomba niondoke, nikajaribu kushinda sehemu nyingine.”

Hivo ndivyo Henry alivofika Barcelona. Alienda kutwaa la liga mbili na UEFA mwaka 2009. Mpaka leo Henry anadai kuondoka Arsenal ndiyo maamuzi magumu kuwahi kuyafanya katika maisha yake. Si rahisi kuagana na watu mliowekana moyoni kwa ajili ya mafanikio binafsi.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

soma zaidi

43 Komentara

    Aubameyang kasikai Call wahuni wanasema , Ngoja tuone nini ataamua kwenye career yake

    Jibu

    Kweli kabisa henry alikuwa anauzalendo na timu yake na kumuheshimu sana kocha wake Wenger ila naona kama anampa Congo Pierre kwa kutaka kusepa klabuni hapo

    Jibu

    Mamuzi yake yalikuwa mazuri Henry kwalicho kiamua kutimukia Barcelona alikuwa mpamba naji Sana namuherewa sana

    Jibu

    Henry akikuwa MTU mwenye uzalendo na timu yake

    Jibu

    Henry Alikipiga sana Enzi zake#Meridianbettz

    Jibu

    Maamuzi yake yalikua mazuri Henry kwa alicho kiamua kutumikia barcelona#Meridianbettz

    Jibu

    kweli kabisa Henry huo ulikua ni uamuzi mgumu na ni wachache sana wenye moyo kama wako

    Jibu

    Henry alikuwa mtu mwenye uwezo kipindi hicho na kipaji

    Jibu

    Daaah..!ulikua wakati mgumu sana kwa Wenger kipindi kile. Sizani kama arsenal watamuachia aubameyang asepe klabuni pale

    Jibu

    Henry akikuwa MTU mwenye uzalendo na timu yake

    Jibu

    Mi nadhani hata auba kwa umri aliokua nao anafikilia kwenda sahemu nyingine kutimiza ndoto zake.

    Jibu

    Aubameyang bado hajafikia uwezo wa kujitolea aliokuwa nao Henry#meridianbettz

    Jibu

    Wamuacha auba aende sehemu nyingine akatimize ndoto zake

    Jibu

    Henry alikua mtu mbaya sana Enzi zake

    Jibu

    Mambo ya zamanii yanakupa historia. Henry alikuwa fitii mno

    Jibu

    Yupo fiti sana

    Jibu

    Sioni ata uwezo wake

    Jibu

    Bonge la makala

    Jibu

    Henry alikuwa na moyo wa peke ake

    Jibu

    Kazi ipo

    Jibu

    Auba ndio mshambuliaji alieipaisha arsenal msimu huu

    Jibu

    Duh makala noma sana hiiii

    Jibu

    Herny alikuwa mwenye uwezo kipindi hicho

    Jibu

    Kazi ipo

    Jibu

    Mashabiki tunashukuru kwa makala
    @meridianbettz

    Jibu

    Henry alikua vizuri sana

    Jibu

    Hii makala inatufundisha kwamba husimzarau mtu usiyemjua.

    Jibu

    My fav player of all time

    Jibu

    Hiyo ndo waswahili wanasema usimzarau mtu usiemjua ,au hutakiwi kujitangaza vitendo vyako ndo vitawahabarisha hata asiekujua jina lakini kitendo chako tu atajua ,si yule aliefanya kitu flani ?

    Jibu

    Sasa hapa Henry anamfundisha vibaya aubameyang nae afanye maamuz ya kuondoka Arsenal me namshauri asipokee simu

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

    Aubameyang kwa sasa hawezi kuondoka arsenal

    Jibu

    Hee sio poa

    Jibu

    Jeshi LA zamani

    Jibu

    Safi sana tumeona hata kwa roben van persie vile vile kaja united kanyayua ndoo

    Jibu

    Habari nzuri sana

    Jibu

    Habari njemaaa

    Jibu

    Yuko sahihi kabisah Henry

    Jibu

    Mi nadhani hata auba kwa umri aliokua nao anafikilia kwenda sahemu nyingine kutimiza ndoto zake.

    Jibu

    henry alikuwa na moyo wa kipekee sana ukiacha mbali na kipaji chake atakumbukwa sana pale barcelona

    Jibu

    Kila mchezaji hua ana ndoto kwenye career yake ya mpira.

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.