Hernández Kutua Munich

Bayern Munich nao hawajawa kwenye ubora wao katika siku za usoni kitu ambacho bado kinawapa nafasi ya kufanya vibaya kwenye michuano mbalimbali wanayoshiriki. Ikumbukwe Bayern alikuwa kisiki cha ushindani akileta upinzani wa aina yake hata kwa klabu zenye historia kubwa lakini sasa amepotea kabisa kwenye ramani na kuwa klabu inayoruhusu wapinzani kuchukua alama kwake kwa urahisi sana.

Uwepo wa jambo hilo inapelekea kikosi hicho kifanye usajili ili kujikinga na wimbi hilo la kupiteza alama katika hali isiyokuwa na ulazima; isitoshe kwa sasa wanahitaji heshima kwa kujijenga upya. Mbali na hilo kwa sasa wanahitaji wachezaji ambao tayari wapo katika viwango vyao vya juu kutokana na kuwa na wachezaji ambao umri wao kwa sasa umesogea sana na wangehitaji wachezaji hao waweze kupata nafasi ya kupumzika.

Nyota kama Robben, Muller, Ribery na Nuer umri wao kwa sasa umesogea hivyo hawana budi kuangalia damu changa. Lucas Hernández ametimka kutoka Hispania na kujiunga na miamba hao kwa msimu ujao ikiwa ripoti za awali zinaonesha kwamba mchezaji huyo alifikia hatua za makubaliano ya awali wiki kadhaa zilizopita na sasa amejiunga na kikosi hicho kwa fungu nono la €80m ikiwa ni sehemu ya ada ya kumuachia huru mchezaji huyo kuondoka.

Hernández Kutua Munich

Mara ya kwanza alikuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United lakini inaonekana mipango ya awali ya klabu hiyo ilikawia kuingia njiani na ndiyo sababu ya kufanya jambo hilo likawie sana hadi kuwahiwa na Wajerumani hao. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba amesaini mkataba wa takribani miaka minne au mitano ili kuweza kutoa huduma kikosini hapo.

Usajili wa Hernández’ utakuwa umevunja rekodi kwa klabu hiyo tangu ufanywe 2017 kwa Tolisso alipojiunga kutoka Lyon kwa ada ya €41.5. Jambo hilo litakuwa la kihistoria kwa klabu hiyo. Munich atakuwa anajiimarisha vizuri kwenye ligi yao na michuano mingine iliyo mbele yao kwa kufanya usajili huu.

Mwanzo ilikuwa na dalili za awali kabisa kwa msimu uliopita walipokuwa wanawavizia nyota wawili wa Ufaransa ambao ni Pavard na Hernándeź na kama ilivyo ada, kocha wa kikosi hicho anategemewa kumegewa fungu la €200m ili kufanya usajili mzito kikosini hapo.

Kuna maingizo mapya kikosini hapo pia upande wa pili kuna nyota ambao wakati wao wa kuendelea kusalia klabuni hapo unaingiwa na walakini. Baadhi yao ni Renato Sanches ambaye hajapata nafasi kabisa msimu huu pamoja na kuwa ni kijana mwenye upekee.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Iko poa

    Jibu

Acha ujumbe