Ander Herrera amesisitiza kuwa Mbappe na Neymar wanafuraha sana pale PSG na klabu haina mpango wa kuwauza, zaidi ya kuwanunua mastaa wengine.
Mbappe na Neymar, kwa pamoja wamekuwa wakihusishwa na kuondoka klabuni hapo, huku klabu za Real Madrid na Barcelona zikihusishwa zaidi kuwania saini zao.
Lakini kwa mujibu wa Herrera, fowadi hawa wanaonekana kuwa na furaha zaidi pale PSG baada ya kuwasaidia timu yao kuchukua ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya 3 mfululizo.
Herrera akizungumza na AS, aliulizwa pia ikiwa klabu ikalazimika kumuuza mmoja wao, ni yupi kati ya wawili hawa itakuwa siyo rahisi kumbakiza?

“Sifahamu, kwa kuwa sielewi wanalipwa kiasi gani au ni mapato ya kiasi gani wanayoiingizia klabu, ambayo pia ni kampuni.”
“Lakini nafahamu kuwa wao ni sehemu muhimu zaidi katika mradi na ninawaona wanafurahia kuwa na PSG.” -Ander Herrera
Ikumbukwe PSG walimshusha Neymar klabuni hapo kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya €222M akitokea Barcelona mwaka 2017. Na sasa Barcelona wanataka kumrejesha kondoo waliyemuuza kwa mkulima mwingine wakiona bado amenona.
Wakati huo Mbappe alijiunga na klabu hiyo mwaka uliofuata baada ya Neymar kwa mkataba wa kudumu akitokea Monaco kwa ada ya €135M.
Wamekuwa sehemu muhimu ya PSG, na PSG wana jeuri ya pesa kuendelea kuwabakiza klabuni hapo licha ya kuripotiwa kwa nyakati tofauti kuwa mastaa hao wanatamani kuondoka.
Unafikiri PSG wamuuze nani na kumuacha yupi? Nitafurahi kusoma maoni yako hapo chini.
Bashiri Mechi za Leo Bundesliga BETI HAPA



Neema juma
Km wanafuraha wote wawili kuwepo PSG wawaache tu mpk watakapoamua wenyewe kuondoka
Rehema
Nafkili waache wote hapo PSG had watakapoana muda wao umeisha
Agness
Safi Sana Kama wanafurahi waendee kubaki hukohuko
Mwanaidi
Ni vizuri sana wakiwa na furaha
Tahiya
Muunganiko wao ni mzuri itakuwa Poaw
Hope mwaikuka
Wabak hapo hapo tu
Ester jackson
Mwamba wawili wamekutana sasa PSG mambo mubashara wapizani mjipange sasa
Antony Luseno
Kuwa na furaha ni jambo la msingi ila waonyeshe uwezo wao kutokana na viwango kushuka has a kwa Neymar
Evaluziga
Kama wanafuraha waendelee kukaa hukohuko
felister
kama kumuuza wamuuze mbappe wamuache neymar ila mm Kama mm ningependa wote wabakie apo apo PSG
Emmy cleopa
Wabaki tu
Salma
Kama wana furaha wabaki hapo hapo
Theckla
Hamna wakumuuza nafurahi kuona wanamfanya kazi pamoja
Rehema Dickson
Ni kweli wanafuraha na walipo kwa sasa na ndo maana wana fanya vizuri mtu anatakiwa kufurahia alicho nacho na alipo kwa wakati huo ili mambo yawe sawa
mathayo sonje
ni kweli kabisa neymar na mbappe ni sehemu muhimu sana pale PSG na ndomana hawataki kuwaachia
winfrida
PSG wana jeuri ya pesa kuendelea kuwabakiza klabuni hapo
isha
Wasiende popote wabaki wawe pamoja
Devotha
Wameipa heshima zaidi PSG hawajutii kuwa pale ndo maana wanafurahia kuwepo
Warda
Wote wauzwe tu mie sina hata faida#Meridianbettz
Adelta
Safi Sana waendelee kukaa
PSG
Elika
Hao ni kama mapacha 3..hawana sababu ya kwenda popote..hapo psg ndo furaha yao
Adelta
Safi Sana waendelee kukaa PSG
Khadija
Wauzwe tuu sina faida nao#meridianbettz
Evaluziga
Safi sana waendelee kukaa psg
Mwajuma
Kwa mtazamo wake yeye anawaona wana furaha lakini nikweli neymar hana fraha pale PSG
Asha mvugalo
Gud news
Isaya massawe
Mbape angeenda Madrid ingekua poa sana
Sadick
Ander Herrera angekumbuka msemo wa Waswahili unaosema usiusemee moyo. Naamini Mbappe na Neymar wakipata timu kubwa inayoweza kuwanunua wanahama#meridianbettz
mwakalosi
herrera asiwasemee watu bhn
Ester mmakasa
Me sitaki auzwe mchezaji yeyote kati yao kwasababu wote wako kwenye nafasi nzuri na wala hawana mpinzani.
Christopher
Waendelee tu kubakia hapo ambapo ushindan ni wa kawaida majukumu yao sio makubwa sana ukilinganisha na timu kama Manchester united etc
Hamidu
Mafundi wa mpira#meridianbettz
Aziza mushi
Ni vizuri Sana Kama wanakuwa na furaha
David Pere
Mbape kweli fraha anayo lakini si kwa Neymar Hana furaha pale Ndio maana anataka kuondoka
Povel
Gud Kama wataendeleah kusalia kwny viunga hvy vya prince stadium
Gabriel
Haya ndo majembe yanayoisimamisha Chelsea
Gabriel
Haya ndo majembe yanayoisimamisha PSG
JULIANA
Hiyo ni jeuri ya pesa,ndiomaana wako na furaha
Mwanahamisi
Wabaki tuu
Amani
Wamekuwa sehemu muhimu ya PSG lazima wafurahie na kujivunia viwango vyao#meridianbettz
lombo
gud newz asante
Genia Sikaluzwe
Ni vema ukabaki tu hapo hapo
Caroline
Wanapenda timu yao
Magdalena
PSG kumenoga wababe wawili kukutana katika timu moja
Zeiyana
Sizani kama PSG itakua tayali kuwauza mastaa hao
Lydia Emmanuel Magoti
Wapo vizuri wanajua Nini wanakifanya ndomana wanajikuba Sana Fundi mpila awaoneani kinyongo awanyimiani pasi
Kenani
Safi Sana soccer lenye mafanikio linaleta matumaini uwanjani
Theonestina
Wote wako vizur.nawakubar
Mariam mtandama
Habari mjema
Samiah
Nihabari njema sana hz
Dorophina
Mafundi wa mpira wabaki waendelee kuiinua PSG
Shafii
Makala bomba na meridianbet
Asia Abdy
Tunategemea makubwa kutoka kwao
Fatina mfingi
Ni habar nzur