Ni ngumu kumchukia yule unayempenda, hata akikupa sababu za kumchukia bado utaendelea kumpenda maana upendo hudumu na kuvumilia yote
Paul Labile Pogba katika kichwa chake ana ramani nzima ya Manchester united namna inavyotakiwa kucheza kwa sasa, ni siri ambayo inaishi katika kichwa chake, utaiona pale tu miguu yake ikiwa inakanyaga nyasi za Old Trafford.

Katika dimba la kati la Manchester united anaichora mipango yote ya mashambulizi ya timu, kuna tofauti kubwa sana ya Manchester united ikiwa na Pogba uwanjani na ile ambayo haina Pogba uwanjani.
Yenye Pogba uwanjani inachangamka sana katikati, timu inapanda kupitia miguu ya Pogba, ni rahisi kumwona mshambuliaji Anthony Martial akiokota mpira baada ya kufunga goli tamu lenye pasi ya miguu ya Pogba.
Ana umuhimu mkubwa uwanjani, Manchester United isipokuwa na Pogba uwanjani kuna ufundi unapungua wanapata shida sana kushinda.
Uzuri wa pogba ana uwezo wa kucheza maeneo muhimu yote ya kiungo itategemea kocha anamtaka kwa matumizi yapi, akicheza kama kiungo mchezeshaji ni kama vile unakitazama kiuno cha shakira katika vazi lake laini.
Anasukuma mipira mbele kwa kasi ya ajabu, akicheza kama kiungo mshambuliaji ni kama kumpa mchawi mtoto akulele, Pogba hapa anapiga mashuti golini kisha anatoa assist kizuri zaidi anakupa na kufunga pia.

Yote haya yanapatikana katika kichwa chake, mashabiki wanalitambua hilo, licha ya mambo yote aliyoyafanya bado wamefunga macho na mdomo wakiamini wanamhitaji zaidi kuliko anavyowahitaji.
Alitamka wazi anataka kuondoka Manchester United, bodi ya timu wakaweka pamba masikioni naamini hawakusikia hilo.
Kwa sasa jina lake na Bruno Fernandes ndiyo habari ya mjini kila mtu anazungumzia kuhusu hilo, wamepata sababu ya kumpenda tena, ndivyo maisha yalivyo.
Paul Pogba anabakia kuwa mchezaji mzuri ambaye kila timu inatamani kuwa naye, siwashangai Manchester united kuamua kufunga macho katika hili.


Povel
Thnks kwa update za michezo
Hope mwaikuka
Ni mchezaj sana ila nyota hana
Njiku
Pogba no mchezaji mzuri sana licha ya mashabiki wa man u kumsahahu pobga kutokana na majereha pia na timu kufanya vizuri kwa ujio wa Bruno,pobga anafanya vizuri sana alivyorejea kikosi hapo pia kusababisha penati dhidi ya Tottenham na game kuisha sare ya moja moja pia Pogba anakupa vitu vingi sana akiwa uwanjani maana anatoa pasi za mwisho pia anafunga Paul pobga atabaki kuwa bora kwa man u
Devotha
Pogba ni mchezaji mzuri sana! Asante #meridianbet kwa taarifa
Amiri Kayera
Ni mchezaji alieanzia hap soka lake kisha akaondok sasa kalud km mfalme pale United
Gabriel
Paul Pogba amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Manchester United, amekuwa na mapenzi ya dhati na klabu na kujitahidi kucheza kadri ya uwezo wake. Uchezaji wake ulitetereka kidogo wakati uhusiano wake kuyumba dhidi aliyekuwa meneja Jose Mourinho. Ujio wa Ole Gunnar umekuwa na kama chachu ya jitihada zaidi za kiungo huyu,. ambaye alionesha ubora wa hali ya juu. Unaweza juwa namna gani mashabiki wa Man U wanavyomkosea staa huyu Mashabiki wa Man U, kama mashabiki wa timu nyingine yeyote hawapendezwi na kufanya vibaya kwa klabu yao. Licha ya klabu hiyo kuwa na kuwa na matarajio ya kutia jitihada ili waweze kumaliza katika 4 bora baada ya kuanza vibaya msimu, bado Man U hawakuweza kutimiza adhma hiyo. Mashabiki wamekuwa wakimshambulia zaidi kwa lugha ya kejeli na kudai Ole Gunnar amuondoe klabuni hapo.
Mashabiki wa United wanaweza kuwa wanasahau kuwa Paul Pogba alikuwa mmoja wa wachezaji ambao walikuwa wanategemewa zaidi kwa Man U kupata matokeo mazuri, uwezo wake wa kulinda, kuwa kiungo na kushambulia ulimfanya aweze kuchukua majukumu mbalimbali katika timu kulingana na aina ya mchezo na maamuzi ya meneja. Msimu huu uliopita Pogba amefunga magoli 16, na asisti 11 kwenye gemu 47 za michuano yote.
Man U wanaweza kumpoteza staa huyu ambaye anahusishwa zaidi na Madrid, Zidane anamtaja nyota huyu kama staa ambaye anaweza kufanya majukumu zaidi ya moja kulinda, kushambulia na kutulia kwenye nafasi yake kama kiungo ukiacha uwezo wake wa kupata magoli.
Baadhi ya mashabiki wanashindwa kutambua au kama sio wanapuuza mchango wa nyota huyu katika mshike mshike wa msimu ulioisha na misimu mingine iliyopita. Kwa wanao tambua mchango wake vyema, bila shaka wangempa heshima anayostahili!
Sabrina
Maoni:Poul Pogba jeshiii ni muhimu pale man u
Furahav
Ata mimi namkubali sana.
neema hassan
Mchezaji mzuri sana
Omary lukumbi
Kwa paul pogba n mchezaj hatar sana kiungo muhimu sana kwenye kikosi cha man United ana miliki mpira kasi uwanjan pasi hatar na mtu wa burudan akiwa na beki anaemkaba hajiamin piq ni zao la man United
Theonestina
Pogba tunamtegemea sana.
Edgar
yupo vizuri sema daah sijuagi kwa nini hana kismart kabisa
Aziza mushi
Namkubali Sana pogba
Revina
Pogba ni Mchezaji ambae anajituma lakini hana bahati sema ni mtu mmoja makini sana na ni mtu mwenye furaha ya aina yake hata akiwa kwenye familia yake
farida ahmadi
Pogba ni mchezaji mzuri Sana pia hata mashabiki wake tunafurah kusikia mamb mazuri km hayo
Shafii
Gud newz
Mwanaidi
Pogba ndio mchezaji pekee anayeangaliwa man u yupo vizuri amezidi kuiva dogo
Evaluziga
Namkubali Sana pogba
David Pere
Heshima yake ipo sanaa inabidi atulize kichwa akili take iwepo pale aendelee kuleta burudani kwa mashabiki wake na Man U kwa unumla
Salma
Mchezaji mzuri sana
Theckla
Paul Pogba anabakia kuwa mchezaji mzuri ambaye kila timu inatamani kuwa naye
Tahiya
Paul Pogba ni mchezaji mzur ndio mana usajir wake ulikuwa juu
mwakalosi
huyu pogba alitusumbua sana aisee yaan kila week yeye ndio anamake headline tu sasa ngebe kwisha
jullie
yuko vizuri jamaa
Frank Patrick
Washabiki wa Man u wameanza kumuelewa tena
Mwajuma
Talent player
warda
Sasa Tukiacha Pogba aondoke Tutabaki na nani Rash ndo anainuka#Meridianbettz
Johnmary joel
Nimchezaji mzuri sana#meridianbett
Hamidu
Kiungo fundi#meridianbettz
felister
uzuri wa pogba anaweza kucheza maeneo mazuri yote ya kiungo
Magdalena
Pogba amekuwa na mchango mkubwa Sana manchester United anastahili heshima kubwa
Tatu
Pogba ni mchezaji mnzuri sana kwa man
Genia Sikaluzwe
Pogba amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye timu Manchester united
Mwanahamisi
Hata mm namkubali sana
Dorophina
Pogba yupo vizuri na yupo makini zaid akiwa uwanjani wajitahidi man u wasimpoteze
Lydia Emmanuel Magoti
Pogba nimchezaji muhimu wa man U anajua kuitumikia kazi yake kipasavyo
Sadick
Anachotakiwa Pogba ni kuwa na mapenzi na timu na kuondokana wakala wake mbinafsi #meridianbettz
Mariam mtandama
Mchezaji mzur sana
Caroline
Pogba ni mchezaji Mzuri kila timu inataka kua nae
lombo
pogba inabid atoke man u ili akaanze maisha mapya kama mwenzake
isha
Pogba yuko vizuri namkubali
Ester jackson
Paul Pogba amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Manchester United, amekuwa na mapenzi ya dhati na klabu na kujitahidi kucheza kadri ya uwezo wake licha ya majeraha yake ya Mara kwa Mara .
Flomena
Alitamka wazi anataka kuondoka Manchester United, bodi ya timu wakaweka pamba masikioni naamini hawakusikia hilo.
Khadija
Kiungo fundi#meridianbettz
Sylvester
Pogba Mnyama alierudi kwa morali ya juu toka alipoumia na natumaini atafanya vizuri sana kwa muunganiko na Fernandes
Sylvester
👌👌👌👌👌👌👌👌
Zeiyana
Paul pogba alikua mmoja wa wachezaji ambao walikua wanategemewa zaidi kwa man u kupata matokeo mazuri
Christopher
Tokea amerudi uwanjani ameonyesha kiwango kikubwa sana
Ernest
Nafurahi kuona mashabiki wa Man U wanatambua thamani na mchango wa Pogba ndani ya Man U.
Asia Abdy
Pogba ana uwezo
Issa
Pogba
Fatuma kasomo
Tokea amerudi uwanjani amwinyesha mambo mzuri
Rehema
Namkubali sn
Neema juma
Pogba ni kiungo mzuri sana
Samiah
Pogba namkubali sanaaa
Angelina
Mchezaji bora pogba
Hakuna Timu Bora Kama Man U Kwa Sasa – Gary Naville
[…] Manchester United wakiendelea kugawa dozi kwa wapinzani wao kwenye Ligi kuu ya Uingereza mkongwe wao mmoja […]