Huwezi Amini Kama Walikuwa Madrid

Huwa ni ndoto ya kila mchezaji kujikuta anacheza soka lake katika klabu zenye majina makubwa kama Real Madrid, Barcelona, Man City, United; pale inapotokea wanapata ofa za kujiunga nazo ni wacheche sana huchomoa ofa hizo kwa kukataa kujiunga nazo. Hii inatokana na masuala ya kimaslahi au hata ufahari kujiunga nazo.

Kuna wachezaji ambao wameweza kuichezea Madrid ambao kwa sasa ji maadui wakubwa tena kwa upandw mwingine katika vikosi hivyo pindi vinapokutana uwanjani. Hii haiangalii kwamba klabu hiyo hapo awali ndiyo ilitambua vipaji vyao na kujitahidi kuviendeleza ili visiweze kupotelea tu mtoni.

Saul Niguez

Alijiunga na Madrid akiwa na miaka 11 na wakati huo ilikuwa mwaka 2006; aliweza kutimka klabuni hapo akiwa na umri wa miaka 13 . Mchezaji huyo aliweza kuichezea timu ya wakubwa mwaka 2012 hapo ndipi akaanza kuonesha thamani yake rasmi katika uga wa soka barani Ulaya. Na baadaye akaweza kutimka katika ardhi hiyo na kujiunga na mahasimu wao Atletico.

Fabinho

Kwa sasa ni mchezaji mahiri kabisa wa Liverpool lakini historia yake kubwa ilianzia akiwa Hispania ambako ndiko aliweza kuonekana kama ana kitu cha kipekee ambacho angeweza kukiongeza katika soka. Aliweza kucheza mechi zake 30 akiwa ndani ya taifa hilo la Hispania ndsni ya viwanja vya Madrid. Uwezo wake ukaanza kuwavutia wengine ndipo safari yake ilipokwiva na kuamua kutimka.

Filipe Luis

Damu hii ya Brazil ilianza soka lake katika kikosi cha Figuirense na baadaye kuonekana kama ana kitu kipya cha kuongeza ndani ya taifa la Uhispania ndipo Madrid walipovutiwa naye na kumpa mkataba. Lakini soka ni mchezo wa biashara; baada ya kukaa naye kwa kipindi wakaweza kumwachia  mchezaji huyo na kujiunga na Atletico pia.

Juanfran

Pamoja na kuonekana ni mkongwe ndani ya kikosi cha Atletico, lakini ameweza kucheza katika viwanja vya matajiri hao kama mchezaji ambaye alianza kung’arisha njia zake akiwa na vikosi hivyo. Lakini aliweza kutimka kujiunga na upande wa pili akitokea kikosi cha Madrid B baada ya kuona sasa kuna kitu angeweza kukiongeza katika klabu nyingine kama Osasuna kabla ya kujiunga na Atletico.

Atletico na Real Madrid wanaonekana kuwa na mikataba mizuri ya kibiashara kutokana na kuuziana idadi kubwa sana ya wachezaji ambao ni wa muhimu sana katika vikosi vyao; ambao baadae hugeuka kuwa mahasimu wao tena.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.