Leeds United imepanga kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Korea Hwang-Hee- Chan kama mbadala wa Daniel James endapo ataamua kuondoka klabuni hapo.

James amekuwa akiwindwa na vilabu vingi ikiwemo Manchester United na Southampton lakini bado inaeonekana milango ni migumu kwa mchezaji huyo kuondoka.

Hwang, mshambuliaji wa Wolverhampton Wanderers, amekuwa kiungo hodari zaidi katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifanya kazi na Marsch katika klabu ya Red Bull Salzburg.

“Ninamjua Hee-chan vizuri, ninampenda Hee-chan, analijua soka letu naweza kusema amekuwa kwenye orodha yetu tangu mwanzo.” Marsch alisema.

