Muda wa Isco Alarcon klabuni Real Madrid unaonekana kufika ukingoni wakati staa huyu akionekana kupoteza radha kwenye kikosi cha Real Madrid.
Ripoti zinataja kuwa staa huyu tayari ameshafahamu hatma yake klanuni hapo.
Isco Alarcon anamaliza mkataba wake wa sasa na Real Madrid mwisho wa msimu huu, bila shaka tayari ataanza kutazama uelekeo baada ya hapo.
Kwa mujibu wa Marca, staa huyu kwa muda sasa amekuwa akifahamu kuwa klabu yake haipo tayari kumuongezea mkataba baada ya kumaliza mkataba wa sasa.

Isco Alarcon tayari kwa sasa anaweza kufanya mazungumzo ya makubaliano ya awali na vilabu vya nje ya Hispania kuelekea kiangazi.
Mpaka sasa, Isco hajafanya makubaliano ya awali na klabu yeyote na anatarajiwa kuendelea kuwa Real Madrid kwa sehemu ya msimu iliyobakia.
Isco Alarcon anatarajia kufungasha vilago vyake mara baada ya kukamilisha msimu kuelekea klabu ambayo atakuwa ameipata wakati huo. Staa huyo ameshindwa kuwa kwenye kiwango kinachotarajiwa na Real kwa muda sasa.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


