Barcelona Yamuongeza Mkataba Umtiti Mpaka 2026

Klabu ya Barcelona imemuongeza kandarasi mpya mlinzi wao Samuel Umtiti ambapo kwenye makubaliano mapya Umtiti amekubali kupunguzwa kwa mshahara wake na dili hiyo itadumu mpaka mwaka 2026.

Beki huyo wa kati wa Ufaransa hajatumiwa sana na klabu hiyo msimu huu, lakini alikuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Camp Nou, jambo ambalo lilifanya kumuuza kuwa ngumu.

Mshahara wa Umtiti umepunguzwa kwa asilimia 10, na mchezaji huyo anaamini kuwa chini ya Xavi Hernandez anaweza tena kuwa mchezaji muhimu kwa klabu.

“FC Barcelona inatoa hadharani shukrani zake kwa Samuel Umtiti kwa juhudi na mapenzi ambayo ameonyesha kwa klabu,” taarifa ya Barcelona ilisoma.

“Kwa kuongeza mkataba huu, Barcelona wanapanua ‘fair play’ na wataweza kumsajili Ferran Torres.

“Beki huyo wa Ufaransa amepunguza sehemu ya mshahara aliyokuwa akipokea kwa mwaka mmoja na nusu ambao alikuwa amebakisha kwenye mkataba wake.

Barca wanajiandaa kuumana na Real Madrid katika nusu fainali ya Supercopa de Espana ambayo itapigwa katika ardhi ya Saudi Arabia siku ya Jumatano ikiwa ni mara ya kwanza kwa El Classico kuchezwa nchini humo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.